Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

687ab161d84a5ced9fcf40dc31f36b60.jpg
 
INAWEZEKANA Bwana mmoja akiwa katika hifadhi ya wanyama, alistaajabu kuona Tembo wakiwa wametulia sehemu moja, kwa muda mrefu ilhali hawajafungiwa kwenye vibanda madhubuti wala hawajafungwa minyororo. Kilichowazuia wasizagae na hata kutotoroka kambini, ilikuwa ni kipande tu cha kamba ambacho, kila mmoja alifungwa mguuni. Tembo ni mnyama mwenye nguvu sana, anayeweza hata kuvunja ukuta. Sasa kilicho mstaajabisha mtalii yule, ni kuona Tembo wale wanashindwa kutumia nguvu zao, kukata kamba na kutokomea mtaani. Akiwa ameshikwa na wahaka wa kutaka kupata majibu, ilimlazimu kumuuliza mkufunzi aliyekuwa karibu, kwanini Tembo wamesimama tu pale bila kukata kamba na kuondoka. Mkufunzi alimjibu: "Kipindi Tembo wanapokuwa wadogo kabisa, huwa tunatumia kamba hizohizo kuwafunga ili wasizagae. Wakiwa katika umri huo mdogo, kamba hizo hutosha kuwadhibiti. Na kadiri wanavyoendelea kukuwa, hukuwa wakiamini kwamba, kamba ile ingali na uwezo wa kuwazua mahala hapo, hivyo fikra zao ndizo huwazuia hata wasijaribu kukata kamba na kuondoka." Sababu ya msingi, Tembo kushindwa kukata kamba na kutokomea, ni ile fikra waliyokuwa nayo kwamba HAWAWEZI kukata kamba na kutoka eneo lile. Hivyo, FUNZO la hadithi hii ni kwamba; bila kujali ni vizuizi vingapi vinavyokuzuia kupiga hatua, endelea kupambana ukijaribu hatua kadha wa kadha kuyafikia mafanikio. Huenda uwezo unao ila umeathiriwa na fikra kama za wale Tembo. Kuamini HAIWEZEKANI kupiga hatua ni sumu, na kuamini INAWEZEKANA ni kujitanzua katika vizui ni nusu ya mafanikio
 
UKUMBUKWE KWA LIPI? Takribani miaka mia moja iliyopita, mtu mmoja alikuwa akisoma gazeti litokalo kila asubuhi. Kwa mshangao na wahka mkubwa, aliona kwenye gazeti hilo, jina lake likiwa limechapishwa katika safu ya Tanzia. (Tanzia ni wasifu wa mtu aliyekufa). Gazeti hilo la kila asubuhi, lilichapisha taarifa ya kifo cha mtu mwingine, huku jina la mtu huyo likichapishwa kimakosa. Awali, alipatwa na mshituko mkubwa; akijiuliza, hivi nimekufa kweli, au? Na aliporejewa na utulivu wa nafsi, fikara ya pili ikawa ni kuona namna alivyozungumziwa na watu waluoamini kuwa amekufa kweli. . Tanzia katika gazeti hilo ilisomeka kama hivi: "Mfalme wa milipuko afariki dunia.", huku sehemu nyingine ikisomeka, "Alikuwa ni mfanyabiashara wa kifo!". Kimsingi, mtu huyu alikuwa ni mvumbuzi na muuzaji mkubwa wa milipuko (Mabomu), ambayo hutumiwa kupigania sehemu mbalimbali duniani na kupelekea vifo. Kwa hivi, alipoyasoma maandishi "Mfanyabiashara wa kifo" alitahayari na kujiuliza, "Je, hivi ndivyo nitakumbukwa pindi nitakapokufa kiukweli?". . Baada ya kichwa chake kutaabishwa na fikra juu ya kadhia hiyo, mwishowe alihitimisha mjadala kwamba, hiyo haikuwa njia bora ya kukumbukwa na jamii. Basi tangu siku hiyo, alijitanibu na biashara hiyo, huku akipambana kwa jino na ukucha kuitangaza amani, kwa kauli na vitendo. Mtu huyu aliitwa Alfred Nobel, ambaye leo hii, dunia inamkumbuka kwa ile tuzo kubwa na mashuhuri duniani ya amani ya Nobel (Nobel Prize). . Kama ambavyo Alfred Nobel, baada ya kubahatika kuona utajo mbaya wa jina lake ukisababishwa na mambo afanyayo maisha ni, akajutia na kuazimu kubadilika kabisa na hatimaye kuacha alama na heshima kubwa duniani, nasi tufanye kama yeye. Tusingoje bahati ya kusikia watakavyo tuzungumza jamaa zetu baada ya kutawafu kwetu, bali tujiandae sasa. . Ukifa utaacha hisia gani? Utakumbukwa kwa lipi? Ni upi utakuwa utajo wako? Utakumbukwa kwa upendo na heshima, au kwa uovu na udhalimu? Watu watahuzunika kukukosa, au watashukuru ukiondoka?.
 
Back
Top Bottom