Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Chanzo Cha Kutoelewana Kwingi Kinasababishwa Na Jambo Hili.

Upo muda iwe kazini au katika maisha yetu ya kawaida, kunakuwa na kutokuelewana sana kati yako wewe na wale wanaokuzunguka. Kwa mfano, unakuta maelewano yanakuwa sio mazuri sana na kunakuwa na kupishana kwingi.
 
Umeshawahi kujiuliza nini huwa chanzo cha kutokuelewana vizuri, iwe kwenye familia, kazini au eneo lingine la maisha yetu hali ambayo husababisha migogoro sana. Kwa jinsi ilivyo chanzo kingi cha kutoelewana husababishwa na jambo moja tu, ambalo ni kutokuwaelewa wengine vizuri.
 
Moja ya kitu cha muhimu sana ambacho unatakiwa kuwa nacho kwenye maisha yako ni kuwa na uwezo wa kuwaelewa watu wengine pia ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima. Hiyo yote ni kwa sababu tumeumbwa watu tukiwa wa tofauti, hivyo ni lazima uwaelewe watu wengine.
 
Ni muhimu kujua wewe ni wa tofauti huwezi kufanana na mwingine kwa mambo mengi. Kwa hiyo swala la kuendana na watu wengine jinsi walivyo hutakiwi kupuuza hata kidogo ndio maana tunasema ni muhimu sana kuwaelewa wengine vizuri.
 
Unapowaelewa watu wengine vizuri kabla hujaanza nao kufanya kazi yoyote, inakusaidia sana kukuondolewa wewe msongo wa mawazo na inaondoa kwako migongano ambayo ungekutana nayo bila sababu yoyote.
 
Jaribu kujiuliza ni mara ngapi umepatwa na hasira kwasababu ya jambo ambalo umekuja kugundua kwamba alaa kumbe ilikuwa ni kitu tu cha kutokuelewana. Unapokuja kugundua hivyo unakuwa tayari umepoteza nguvu na muda wako sana.
 
Inahitaji utulivu kidogo ili kuweza kuwaelewa wengine wanataka nini na wewe unataka nini ili mweze kwenda pamoja. Ikiwa itakuwa kinyume ya hapo utaanzisha mgogoro ambao hukutakiwa kuanzisha, lakini kisa ni maelewano mabovu.
 
Unatakiwa kujua ni rahisi tu kugombana na kila mtu ikiwa huwezi kuwaelewa watu vizuri. Uwe na uhakika utagombana na familia yako, utagombana na wenzako kazini na marafiki zako kwa sababu ya kushindwa kuleta maelewanao kati yenu ambayo yalikuwa ni rahisi kueleweka.
 
Kila siku ipo nafasi ya wewe kuweza kujenga uelewa wako kwa wanao kuzunguka. Unakuwa na nafasi ya kujenga maelewano na watu wanaokuzunguka hiyo ni faida kubwa sana kwako ya kudumisha mahusiano.
 
Unapokuwa unaelewa kujenga mahusiano mazuri, elewa haufaidiki wewe tu, hata wanao kuzunguka nao wananaanza kufaidika kwa kulewana kwa ufasaha ambako inakuwa tayari wewe kumekujenga na kukudumisha.
 
Kuanzia leo usikubali uwe chanzo cha mgogoro kwa sababu tu ya kutoelewana. Jenga maelewano mazuri sana karibu katika kila eneo na hiyo itakusadia sana kuweza kuweza kujenga mahusino mazuri na yatakayokupa pia mafaniko kwenye maisha yako.
 
Mbinu Itakayokusaidia Kuwa Karibu Na Wateja Wako Ni Hii.
Miongoni mwa changamoto ambazo huwakabili wafanyabiashara wengi ni kuwapoteza wateja wengi bila wao kujua. Na tatizo hilo huanza kutokana na wafanyabiashara hao kutokuwa na mawasiliano thabiti kati yao na wateja.
 
Nasema hivi nikiwa nina ushahidi wa kutosha kwani mimi binafsi mbinu hiyo imenisaidia kuweza kuwa karibu na wateja wangu na hatimaye naona matunda yake. Ni mbinu ambayo inafanya kazi vizuri sana ukiitumia.
 
Na mbinu hiyo siyo nyingine bali ni kuwa na mawasiliano thabiti baina yako na wetaja wako au kwa lugha ya kitaalamu huitwa ‘customer database’. Customer database ndiyo ambayo hutumiwa na makampuni mbalimbali.
 
Kwa mfano makampuni ya simu hutumia mbinu hii ili kumjuza mteja ujio wa bidhaa, punguzo la bei, au kumjuza mteja taarifa muhimu kuhusu huduma husika. Kwa hiyo taarifa zote za mteja zinakuwa hapo.
 
Na kwa kufanya hivi kumewafanya wateja kupata taarifa sahihi na kwa muda sahihi kuhusu huduma ambayo hutolewa na kampuni husika. Mteja anakuwa hakosi taarifa sahihi kwa sababu anakuwa anatumiwa mara kwa mara.
 
Kwa kuliona hili nimeona ni vyema nawe ukatumia mfumo wa aina hii ili uwe karibu na wateja wako, mawasiliano thabiti huweka ukaribu baina na wateja wako, hii haijalishi ni biashara gani ambayo unaifanya.
 
Bali kitu cha muhimu cha kuzingatia ni kuhakikisha unafanya hivyo ili uwe unawajuza wateja wako kuhusu biashara unayoifanya. Kama kuna mabadiliko yeyote yanayayohusu biashara yeyote unayoifanya basi usisite kuwajuza wateja wako.
 
IMG_3145.JPG

[emoji42][emoji124][emoji124][emoji124]
 
Back
Top Bottom