Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pia inawezekana kua usaili huo mgumu ni moja ya njia zinazotumiwa na kampuni kuchuja maombi ya kazi. Hii hasa inaweza kuwa kweli kama kampuni hiyo inataka mtu mwenye sifa za kutoa huduma kwa wateja. Mara nyingi kwenye soko “maigizo” haya hutokea kama njia ya kuchuja maombi bila wewe kujua, hivyo kuwa makini.
 
Kuwa Mtulivu

Kubaki mtulivu wakati wa mahojiano yaweza kuonekana kama jambo la kawaida, lakini ni jambo gumu. Afisa uajiri mkali anapo kuhoji, ni ngumu kuendelea kuwa makini. Jitahidi utulie na uonyeshe uwezo wako wa kutatua matatizo ili ufaulu usaili huo. Ukiwa umetulia, onyesha ujasiri wako kwa kujielezea vizuri. Hii inaweza kusaidia hata kupunguza ukali wa mahojiano na kukuwezesha kuyamaliza kwa urahisi.
 
Eleza Panapokuwa na Tatizo

Mtazamo wako kuhusu kazi au majibu yako yanaweza yakawa yamemchanganya afisa uajiri. Kama ni hivyo, basi usiogope. Badala yake, jielezee tena kutumia kauli zinazo eleweka. Kauli kama,`’Naomba nikufafanulie hili kiundani?” zianweza kukuokoa kwenye mahojiano. Zitasaidiakuondoa mashaka kwa afisa uajiri ili muweze kuendelea na mahojiano. Wakati mwingine kosa linaweza lisiwe la kwako. Kama ni hivyo basi mwambie afisa uajiri na muombe akuhoji kwa heshima.
 
Elewa Pale Unaposhindwa

Baadhi ya mahojiano ya kazi yanakuwa ni mabovu kiasi kwamba ni ngumu hata kuyamaliza. Unapoona yamezidi ubovu yakatize, kubali kushindwa. Pale unapoona mahojiano ya kazi yanakosa heshima au yanakudhalilisha ni bora kuyaacha. Muda wako na heshima yako vina thamani kubwa. Usikubali vitumike kiholela. Pia unaweza kuwasiliana na kampuni anayotokea afisa uajiri na kutoa maoni yako.
 
Ni rahisi kusingizia mahojiano ya kazi mabovu kuwa ndio chanzo cha kukosa kazi, lakini wewe pia una nafasi ya kuchangia vizuri kwenye mahojiano hayo. Tabia nzuri wakati wa mahojiano, uwezo wa kuwa mtulivu na uwezo wa kujibu maswali kwa ufasaha vitakusaidia kufaulu kwenye mahojiano yoyote yale ya kazi.
 
Dunia (kutoka neno la Kiarabu; wakati mwingine pia: ardhi na kwa neno asili la Kibantu nchi) ni gimba la angani ambapo juu yake tunaishi sisi binadamu na viumbehai wengine wengi, tukipata mahitaji yetu, kuanzia hewa ya kutufaa na maji.
 
Masafa baina yake na jua ni kilomita milioni 150 au kizio astronomia 1. Dunia huchukua siku 365.256 kulizunguka jua, na masaa 23.9345 kuuzunguka mhimili wake na upana wake ni kilomita 12,756.

Dunia huwa na mwezi 1.

Umri wa dunia hukadiriwa kuwa miaka bilioni 4.5[
 
Ni mahali pekee katika ulimwengu panapojulikana kuna uhai ulioaminiwa kuanza miaka bilioni 3.5 iliyopita[3].

Uhai unapatikana kwa spishi milioni 10-14 za viumbe hai pamoja na wanadamu waliokadiriwa kuwa sasa bilioni 7.2
 
Lakini si tufe kamili. Ina uvimbe kidogo kwenye sehemu ya ikweta; ilhali umbali kati ya ncha mbili ni kilomita 12,713 lakini umbali kati ya sehemu za kinyume kwenye ikweta ni km 12,756, yaani kipenyo hiki kinazidi takriban kilomita 43 kipenyo kati ya ncha na ncha. Tofauti hii inasababishwa na mzunguko wa dunia. Kani nje inasukuma sehemu za ikweta nje zaidi. Kwa hiyo mahali duniani palipo karibu zaidi na anga la nje si Mlima Everest kwenye Himalaya bali mlima Chimborazo nchini Ekuador.[5]
 
Kwenye uso wake dunia huwa na tofauti kati ya nusutufe zake mbili. Nusu moja ina eneo kubwa la mabara yaani nchi kavu ambayo ni asilimia 47 ya sehemu hii. Kinyume nusutufe nyingine inafunikwa na maji ya bahari na eneo la nchi kavu ni asilimia 11 pekee za maeneo yake.
 
Kwa jumla dunia ni sayari pekee katika mfumo wa jua yenye maji katika hali ya kiowevu usoni mwake. Bahari kuu ya dunia inashika asilimia 96.5 ya maji yote yaliyopo duniani. Maji ya bahari huwa na asilimia 3.5 chumvi ndani yake.
 
Kwa pamoja maeneo ya maji hufunika 70.7% za uso wa dunia. Nchi kavu huwa na 29.3% na sehemu kubwa ya eneo la nchi kavu ni bara 7 za Asia, Afrika, Amerika Kaskazini, Amerika Kusini, Antarktika, Ulaya na Australia. (Ulaya inaweza kuangaliwa pia kama sehemu ya Asia ikiwa kama rasi yake ya magharibi. Azimio la kutazama Australia kama bara na Greenland kama kisiwa tu ni azimio la hiari si la lazima).
 
Maeneo ya bahari kuu ya dunia kwa kawaida hugawiwa kwa bahari kubwa 3 za Pasifiki, Atlantiki na Bahari Hindi. Sehemu ya chini baharini iko kwenye Mfereji wa Mariana katika Pasifiki (mita 11,034 chini ya UB). Kwa wastani bahari huwa na kina cha mita 3,800.
 
Tumeona dunia ina umbo la mviringo au tufe. Tufe hilo si kipande kimoja kikubwa cha mwamba thabiti. Dunia ina muundo ndani yake. Muundo huo unafanana kiasi na kitunguu, yaani dunia yetu imefanyika kwa matabaka mbalimbali yanayofuatana kutoka nje kwenda ndani. Kila moja lina tabia yake.
 
Kimsingi wataalamu hutofautisha matabaka matatu ambayo ni:

Ganda la dunia
Koti la dunia
Kiini cha dunia
Ganda la dunia ni sehemu imara na uhai wote tunaoujua unapatikana juu yake. Katikati hali ya koti na ya kiini ni ya joto kubwa sana na maada yake hupatikana katika hali ya giligili (si imara, kuyeyushwa). Kila ukiingia ndani dunia inazidi kuwa ya moto mpaka ukifika ndani kabisa daraja ya harara hufikia nyuzi 5000-6000 °C.
 
Matabaka hayo yanafanywa kwa elementi za kikemia ambazo ni feri (chuma) (32,1 %), oksijeni (30,1 %), silisi (15,1 %), magnesi (13,9 %), sulfuri (2,9 %), nikeli (1,8 %), kalsi (1,5 %) na alumini (1,4 %). Mabaki ya 1,2 % ni viwango vidogo vya elementi nyingine. Elementi hizo zinapatikana kwa hali safi au katika kampaundi za elementi.
 
Vipimo vimeonyesha ya kwamba matabaka mawili ya koti na kiini huwa tena na mgawanyiko ndani yake, hivyo matabaka yafuatayo yanaweza kutofautishwa.

Tabaka Kuanzia kilomita
Ganda la nje 0 - 40
Koti la juu 40 - 400
Koti la kati 400 - 900
Koti la chini 650 - 2900
Kiini cha nje 2900 - 5100
Kiini cha ndani 5100-6371
 
Back
Top Bottom