Kiolwa cha angani (pia: gimba la angani, ing. astronomical object au celestial body) ni jina kwa ajili ya vitu vinayopatikana katika anga ya ulimwengu.
Haya yote ni violwa asilia. Vitu angani vilivyotengenezwa na binadamu ni vyombo vya angani ingawa kuna swali kama mabaki kutokana na vyombyo vya angani vilivyovunjika au takataka kutokana safari za angani yanastahili kuitwa kwa neno hili.
Jua ni nyota ambayo ni karibu na dunia yetu kuliko nyota nyingine. Jua ni kitovu cha mfumo wa jua likizungukwa na sayari nane. Dunia yetu ni moja ya sayari hizo katika mfumo wa jua na sayari zake.
Kikemia masi ya jua ni hasa hidrojeni (73%) na heli (25%). Kiasi kinachobaki ni elementi nzito zaidi, kama vile oksijeni, kaboni, chuma na nyingine. Hata kama hizi elementi nzito ni asilimia ndogo tu za masi ya jua, bado zinalingana na mara 5,000 masi ya dunia kutokana na ukubwa wa jua.
Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa jua liliundwa takriban miaka bilioni 4.57 iliyopita kutoka katika gimba kubwa la mawingu lililoundwa na asilimia kubwa za hidrojeni.
Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa jua liliundwa takriban miaka bilioni 4.57 iliyopita kutoka katika gimba kubwa la mawingu lililoundwa na asilimia kubwa za hidrojeni.
Jua linatoa mwanga, joto na mnururisho mwingine wa aina mbalimbali. Sehemu ya mnururisho huu unatoka kwa umbo la vyembe kama protoni na elektroni ambazo kwa jumla hujulikana pia kama upepo wa jua. Masi ya upepo wa jua ni takriban tani moja kwa kila sekunde.[1] Asili ya nishati hii ni mchakato wa myeyungano wa kinyuklia ndani yake. Katika myeyungano huo hidrojeni inabadilishwa kuwa heli. Elementi nyingine zinatokea pia kwa kiasi kidogo. Badiliko kutoka hidrojeni kwenda heli inaachisha nishati inayotoka kwenye jua kwa njia ya mnururisho.
Nishati ya mnururisho huu ni msingi wa maisha ya mimea na viumbe hai katika dunia. Nuru ya jua inabadilishwa na mimea kwa njia ya usanisinuru kuwa nishati ya kikemia inayojenga miili yao itakayokuwa lishe tena ya mimea na wanyama.
Sayari (kwa Kiingereza planet) ni kiolwa kikubwa cha angani linalozunguka jua (au nyota nyingine) na kung'aa kutokana na nuru ya jua iliyoakisiwa, tofauti na nyota na jua zinazong'aa peke yake. Kwa macho inaonekana kama nyota, lakini baada ya kuitazama kwa muda wa mwaka inaonekana inabadilisha mahali pake angani, tofauti na nyota kwa jumla.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.