Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sayari (kwa Kiingereza planet) ni kiolwa kikubwa cha angani linalozunguka jua (au nyota nyingine) na kung'aa kutokana na nuru ya jua iliyoakisiwa, tofauti na nyota na jua zinazong'aa peke yake. Kwa macho inaonekana kama nyota, lakini baada ya kuitazama kwa muda wa mwaka inaonekana inabadilisha mahali pake angani, tofauti na nyota kwa jumla.
 
Jina la Kiswahili "sayari" lina asili yake katika neno la Kiarabu كوكب سيار kaukab sayar "nyota inayotembea" [1]. Neno hili la Kiarabu linalingana au ni tafsiri ya neno la Kigiriki πλανήτης planetes (lenye maana ya "yenye kutembea") ambalo ni asili ya jina "planet" kwa Kiingereza na lugha nyingine za Ulaya.
 
Tangu zamani watazamaji wa anga katika tamaduni mbalimbali walitambua ya kwamba nyota kwa kawaida hukaa mahali pamoja lakini nyota chache zinabadilisha polepole mahali pao kati ya nyota nyingine zikifuata njia zinazorudia kila mwaka. Nyota hizo ziliitwa "nyota zinazotembea".
 
Zamani kulikuwa na sayari 5 tu zilizoonekana angani kwa macho matupu kama nyota zinazobadilisha mahali[2]. Tangu kupatikana kwa mitambo kama darubini miaka 400 iliyopita idadi ya violwa angani vyenye miendo ya pekee imeongezeka sana lakini imeonekana pia kuna tofauti kubwa sana kati ya violwa hivi.
 
Hivyo wataalamu wa Umoja wa kimataifa wa astronomia (IAU) walikubaliana mwaka 2006 kuhusu ufafanuzi wa sayari. Kiolwa cha angani kinahesabiwa kuwa sayari kama kinatimiza masharti matatu:[3]
 
(a) kama linazunguka jua kwenye obiti yake
(b) kama masi na graviti yake zinatosha kufikia umbo linalofanana na tufe
(c) kama ni kiolwa tawala cha obiti yake na hivyo limeondoa violwa vingine kwenye obiti kwa graviti yake.
 
Ufafanuzi huo uliamuliwa kwa kura hata kama wanaastronomia wengine hawakukubali. Azimio hili liliondoa hadhi ya sayari kwa Pluto [4] iliyowahi kutazamwa kuwa sayari katika miaka iliyopita.
 
Wakati mwingine kuna violwa vingine ambavyo vinavyoitwa pia "sayari" ingawa havitoshelezi masharti yote matatu.

Violwa vya angani katika mfumo wa jua letu yenye umbo la kufanana na tufe yasiyolingana na sharti c) huitwa "sayari kibete" - kwa mfano Pluto.
 
Violwa vinavyozunguka nyota nyingine nje ya mfumo wa jua letu, kama yana masi ya kutosha, huitwa "sayari za nje" (ing. exoplanet). Hadi Mei 2016 kuna 2125 zilizotambuliwa [5].
 
Violwa vyenye masi ya sayari ambazo si sehemu ya mfumo wa jua lolote lakini zinapita angani zinazoweza kuitwa sayari bila nyota (ing. wandering planets, starless planets, siku hizi zaitwa pia "planemo").
 
Kwa Kiswahili kuna tofauti kuhusu majina ya sayari kati ya vikundi viwili:

sayari zinazoonekana kwa macho matupu ambazo ni Utaridi, Zuhura, Mirihi, Mshtarii na Zohali. Hizi zilijulikana tangu kale na mabaharia hasa walizitumia kwa kukadiria njia wakiwa baharini mbali na bara. Majina haya yamepokelewa na Waswahili wa Kale kutoka kwa lugha ya Kiarabu pamoja na majina mengi ya nyota.[6] Ila sayari ya pili yaani Zuhura ambayo ni sayari inayong'aa kuliko zote ina pia jina la Kibantu ambayo ni Ng'andu ("mwenye kung'aa). Kwa lugha za Ulaya kama Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani majina ya sayari za jua letu yanatokana na majina ya miungu ya Roma ya Kale au Ugiriki ya Kale.
 
Kwa Kiswahili kuna tofauti kuhusu majina ya sayari kati ya vikundi viwili:

sayari zinazoonekana kwa macho matupu ambazo ni Utaridi, Zuhura, Mirihi, Mshtarii na Zohali. Hizi zilijulikana tangu kale na mabaharia hasa walizitumia kwa kukadiria njia wakiwa baharini mbali na bara. Majina haya yamepokelewa na Waswahili wa Kale kutoka kwa lugha ya Kiarabu pamoja na majina mengi ya nyota.[6] Ila sayari ya pili yaani Zuhura ambayo ni sayari inayong'aa kuliko zote ina pia jina la Kibantu ambayo ni Ng'andu ("mwenye kung'aa). Kwa lugha za Ulaya kama Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani majina ya sayari za jua letu yanatokana na majina ya miungu ya Roma ya Kale au Ugiriki ya Kale.
 
sayari zisizoonekana kwa macho kama Uranus na Neptun pamoja na sayari kibete (Pluto) zilitambuliwa tu bada ya kupatikana kwa mitambo ya darubini. Hatua hii ya kiteknolojia ilitokea Ulaya na hivyo wataalamu wa Ulaya waliendelea katika desturi ya kutumia majina yenye asili katika lugha za kale Kigiriki na Kilatini. Elimu ya sayari hizi za nje zilizokuwa geni kwa mataifa yote mengine ya dunia ilisambaa pamoja na majina ya Kiulaya na hivyo lugha nyingi zinatumia majina haya.
 
Jua letu lina sayari nane ambazo ni Utaridi (Mercurius), Zuhura (pia: Ng'andu; Venus), Dunia yetu (Earth), Mirihi (Mars), Mshtarii (Jupiter), Zohali (Saturnus), Uranus na Neptun. Toka mwaka 1930 hadi Agosti 2006 Pluto ilikuwa ikitambulika kama sayari hivyo kufanya idadi ya sayari zinazojulikana kuwa tisa. Hata hivyo chama chenye mamlaka juu ya masuala ya sayari na nyota, International Astronomical Union kimetangaza rasmi kuwa Pluto si sayari na kuiita sayari kibeti.
 
Sayari tano za Utaridi, Zuhura, Mirihi, Mshtarii na Zohari [7] huonekana kwa macho kama nyota angani. Lakini tangu zamani zilitambuliwa kuwa tofauti kwa sababu hazikai mahali palepale kama nyota ya kawaida bali huhamahama angani. Kutokana na tabia hii zimetazamwa mara nyingi kuwa na nguvu za pekee au hata kuwa miungu. Unajimu umetumia mwendo wa sayari zinazoonekana kwa macho kama msingi muhimu wa makadirio yao.
 
Sayari nyingine katika mfumo wa jua zimetambuliwa tangu kutokea kwa astronomia ya kisayansi kwa darubini. Hizi ni Uranus na Neptun. Katika lugha ya Kiswahili sayari zinazoonekana kwa macho huwa na majina ya asili ya Kiarabu isipokuwa Zuhura ina jina la Kibantu la Ng'andu pamoja na jina la asili ya Kiarabu. Majina mengine ni ya asili ya Kilatini.
 
Back
Top Bottom