Jua letu lina sayari nane ambazo ni Utaridi (Mercurius), Zuhura (pia: Ng'andu; Venus), Dunia yetu (Earth), Mirihi (Mars), Mshtarii (Jupiter), Zohali (Saturnus), Uranus na Neptun. Toka mwaka 1930 hadi Agosti 2006 Pluto ilikuwa ikitambulika kama sayari hivyo kufanya idadi ya sayari zinazojulikana kuwa tisa. Hata hivyo chama chenye mamlaka juu ya masuala ya sayari na nyota, International Astronomical Union kimetangaza rasmi kuwa Pluto si sayari na kuiita sayari kibeti.