Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Njia za kufuata katika utunzaji wa misituː

kupanda miti sehemu iliyokatwa miti
kupunguza kilimo cha kuhamahama
kuzuia uwindaji wa wanyama kwa kuchoma misitu
kuzuia ongezeko la watu katika eneo dogo
kuelimisha jamii juu ya utunzaji misitu
 
Misitu hii iko kwenye kanda ya ikweta duniani kati digrii za longitudo 10° kusini na kaskazini.

Maeneo makubwa yako hasa Brazil katika beseni ya Amazonas, Afrika katika beseni ya mto Kongo, Asia ya Kusini-Mashariki na kaskazini ya Australia.

Misitu hii imepungua sana kutokana na kukatwa kwa miti na upanuzi wa kilimo.
 
Ardhi na matatizo ya kilimo cha kisasa Edit
Misitu ya mvua huonyesha rutba kubwa lakini ardhi yenyewe mara nyingi inakosa rutba.

Hii ni sababu ya kwamba maeneo ya misitu ya mvua hayafai kwa kilimo. Kama miti inakatwa mvua nyingi huondoa minerali za ardhi na kuzipeleka mtoni. Ardhi yenyewe inachoka haraka na baada miaka michache mavuno hupungua kabisa. Hii imeonekana mahali pengi ambako maeneo ya misitu hii yaligeuzwa kuwa mashamba; baada ya miaka michache ya mavono mazuri wakulima waliopata shida ya kudumisha maisha yao. Kwa bahati mbaya mara nyingi wakulima wale wameendelea kukata miti zaidi wakiacha nyuma kanda la nusu-jangwa.

Wenyeji asilia waliolima katika misitu hii walitumia maeneo madogo madogo tu wakihamahama hivyo mashamba yao yalifunikwa kirahisi tena na miti ya karibu iliyozuia uharibifu wa ardhi.
 
Mzunguko wa minerali Edit
Miti na mimea inastawi vizuri kwa sababu majani pamoja na ubao wa miti inayoanguka chini na maiti za wanyama vinaoza katika unyevu haraka na kuwa chakula cha mimea tena. Harakati hii inasaidiwa na aina nyingi za uyoga zinazosaidia kuozesha haraka vitu vyote vyenya asili ya mimea au wanyama
 
Uwingi wa spishi
Imekadiriwa ya kwamba zaidi ya nusu, labda theluthi mbili za spishi zote za mimea na wanyama duniani hupatikana kwenye misiti ya mvua. Mamilioni ya spishi hazikutambuliwa bado.
 
Misitu ya mvua ya kitropiki imeitwa "duka la madawa ya dunia" kwa sababu kiasi kikubwa cha dawa asilia kutokana na mimea imepatikana hapo.
 
Miyombo ni aina za miti inayoitwa na wanabiolojia kwa jina Brachystegia. Jina la Kiswahili linatoka wingi wa jina la Kibemba: "muombo (miombo)", lakini kwa sababu fulani wingi huu umekuwa umoja kwa Kiswahili: "myombo (miyombo)".
 
Miti hii inaunda misitu isiyo minene hasa katika mazingira makavu kiasi ya Afrika ya Mashariki na Kusini hasa katika nchi Zimbabwe, Zambia, Msumbiji, Angola, Tanzania na Malawi. Misitu ya miyombo inafunika maeneo ya kilomita za mraba milioni 5.
 
Misitu ya miyombo humwaga majani wakati wa majira ya ukame kwa kusudi la kuhifadhi maji ndani yao. Kabla ya kuja kwa majira ya mvua huotesha majani mapya. Wakati wa mabadiliko haya majani yanaonyesha rangi za dhahabu na nyekundu zinazopendeza.

Miyombo inayopatikana mara nyingi ni hasa Brachystegia boehmii na B. longifolia.[1]
 
Misitu ya miyombo ni muhimu kwa maisha ya watu wanaoishi karibu nayo wakivuna hapa matunda, asali, kuni na lishe kwa mifugo. Kukatwa kwa miti hii imezidi kutokana na kuongezeka kwa watu na matumizi ya kuni. Utengenezaji wa makaa karibu na barabara kubwa yanayopelekwa mjini ni sababu muhimu. Katika maeneo ambako tumbako hulimwa wakulima wanakata miti mingi mno wakitumia kuni kukausha majani ya tumbako.
 
Miyombo inaota kwenye ardhi isiyo na rutba sana. Hata hivyo misitu ya miyombo ni nyumbani kwa spishi nyingi za wanyama pamoja na ndege wanaoishi hapa pekee. Wanyamapori wengi wanapata kinga na lishe kati ya miti hii kama vile tembo, mbwa mwitu, na wengine.
 
Ubao ni dutu inayofanya gogo na matawi ya mti. Ina matumizi muhimu kwa ujenzi na vifaa pia kama kuni kwa moto.

Ubao hutengenezwa na mti wakati wa kukua. Ubao laini katika ganda la nje la gogo hupitisha maji na lishe kutoka mizizi kwenda kwenye matawi na majani. Kila mwaka ganda jipya linaongezeka nje na ganda la ndani huwa imara na kupoteza uwezo wa kupitisha maji. Mabadiliko haya ya kila mwaka huonekana katika miviringo ya ubao ndani ya mti.
 
Ubao umetumiwa na wanadamu tangu miaka maelfu. Mwanzoni ilitumiwa kama kuni na fimbo ya silaha. Baadaye watu walijifunza kuchonga ubao kwa matumizi mbalimbali kama vile ujenzi, vifaa, sanaa kama uchongaji, karatasi na mengi mengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…