Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ubao huwa na faida ni imara lakini si vigumu ya kukata na kuchonga, tena ni nyepesi. Pia unapatikana kwa wingi angalau katika maeneo ambako miti inakua.
 
Mwanzi ni jina la spishi nyingi za manyasi makubwa yanayoweza kuonekana kama miti. Mianzi yote huwa na shina ya aina ya ubao.

Mianzi hupatikana kiasili katika Afrika, Amerika na Asia lakini inastawi pia ikipandwa Ulaya.
 
Urefu wa spishi kubwa hufikia kina cha mita 40. Inaweza kukua zaidi ya mita 1 kila siku lakini kwa kawaida ni sentimita 3-5 kwa siku.

Shina la mianzi huwa na umbo la bomba na unene wake ni hadi sentimita 30. Shina hugawiwa na vifundo. Kila kifundo kina chipukizi na machipukizi yanaweza kuendelea kuota matawi.
 
Mianzi ina matumizi mengi kwa binadamu. Inafaa kwa ujenzi wa nyumba, madaraja au maboti. Mashina hutumika pia kwa mabomba ya maji katika nyumba na kilimo.
 
Wakati ni changa na laini yaani kabla ya kuwa ubao mwanzi unafaa kama chakula baada ya kupikwa. Mtovu unakusanywa pia kama kinywaji hasa pombe.

Katika utamaduni wa China ya Kale vipande vya mianzi vilitumiwa kama bao za kuandika matini.
 
Mikalatusi au mikalitusi (kwa Kiing. gum tree) ni miti na vichaka ya jenasi Eucalyptus katika familia Myrtaceae.

Miti hii kiasili inatokea Australia na maeneo jirani ya Australasia. Kuna spishi zaidi ya 700 katika jenasi hii. Spishi 15 pekee ziko nje ya Australia. Siku hizi zinapatikana kote duniani kwa sababu zimepandwa kote katika maeneo tropiki na nusutropiki pamoja na Amerika, Afrika, nchi kando la Mediteranea, Mashariki ya Kati, China na Uhindi. Spishi zilizo nyingi haziwezi kustawi katika maeneo penye jalidi (kama halijoto inashuka chini ya sentigredi 0) maana mikalatusi haziwezi kukauka wakati wa baridi na kama halijoto inashuka mno maji katika matawi na shina inaganda na kuharibu seli zake.
 
Spishi mbalimbali zimeenezwa duniani kutokana na tabia zao za kukua haraka na hivyo kuwa chanzo cha ubao, kuwa na mafuta ndani yake yenye manufaa mbalimbali na wezo wao wa kukausha kinamasi na hivyo kupunza hatari ya malaria. Hivyo kuna pia upinzani dhidi ya kupanda mikalatusi kwa sababu zinatumia maji mengi[1].
 
Mikalatusi inapatikana kama vichaka au miti mikubwa hata mikubwa sana.

Mikalatusi za msituni huwa na shina moja ndefu na kilele cha matawi kisicho kirefu sana. Mkalatusi jitu (Eucalyptus regnans) ni mti wa majani mrefu kabisa; mmoja ulipatikana huko Tasmania mwenye urefu wa mita 97 na mzingo wa mita 20.
 
Vichaka vya mikalatusi vinafikia kimo cha chini ya mita 10.

Kimo cha miti yao hupangwa kuwa

midogo — hadimita 10
wastani — mita 10–30
mirefu — mita 30–60
mirefu sana - mita zaidi ya 60
 
Karibu spishi zote huwa na majani mwaka wote lakini chache zinatupa majani wakati wa kiangazi. Kama spishi nyingi za familia ya myrtaceae majani huwa na tezi za mafuta.

Hata miti mikubwa mara nyingi hutoa kivuli kidogo tu kwa sababu majani yanatazama chini kwa kusudi la kupunguza athira ya nuru ya jua kwenye kanda la tropiki.

Majani mapya na majani yenye umri mrefu zaidi mara nyingi huonekana tofauti kwa rangi na umbo.
 
Kwenye spishi mbalimbali tabaka ya nje ya ganda inakauka na kuachana na shina kwa kanda ndefu au kwa vipande-vipande. Spishi nyingine zinashika ganda lililokauka kwenye sehemu ya chini ya shina pekee (kwa Kiingereza inaitwa "black butts" au "half bark"), sehemu ya juu ya shina huwa na ganda nyororo.
 
Mikalatusi huwa na aina ya mafuta ndani ya majani na ubao yanayoweza kuwaka. Kuna taarifa ya kwamba miti ililipuka wakati wa moto ya msituni. Moto zinaweza kuenea haraka kwenye misitu ya mikalatusi kwa sababu ndimi za moto zinaruka katika vilele vya matawi; katika hali ya joto mafuta kwenye majani huyeyuka kuwa mvuke ambako moto inaenea haraka mno.
 
Miti ya mikalatusi zinaweza kudumisha moto kwa sababu baaada ya kuangamizwa nje kuna sehemu za kuotesha majanai na matwi zinzofichwa ndani ya ganda au kwenye sehemu ya mizizi yao. Pia mbegu ni ngumu haiharibiki haraka na kuota baada ya moto kupita.
 
Samaki ni wanyama wenye damu baridi wanaoishi kwenye maji ya mito, mabwawa, maziwa au bahari.

Wote ni vertebrata, yaani huwa na uti wa mgongo.

Wanatumia oksijeni iliyomo ndani ya maji kwa kuyavuta kwenye mashavu yao.
 
Kuna aina nyingi za samaki wadogo wenye urefu wa sentimita moja na wakubwa wenye urefu hadi mita 15. Ila tu viumbe wakubwa kwenye maji si samaki bali nyangumi ambao ni mamalia.
 
Samaki ni chakula bora kwa sababu nyama yake ina protini nyingi inayopokewa kwa urahisi na mwili wa binadamu. Leo hii ni zaidi ya watu bilioni moja wanaotegemea samaki hasa kama chanzo cha protini.
 
Tangu zamani samaki walivuliwa na watu. Wanaoishi karibu na bahari au mito mikubwa mara nyingi ni wavuvi.
 
Mbali na kuvua tu, watu wanafuga samaki pia. Ufugaji samaki hutokea hasa katika mabwawa madogo; samaki wanapewa lishe ili wale na baada ya kufikia ukubwa unaotakiwa maji yanaondolewa kwenye bwawa. Lakini miaka ya nyuma ufugaji samaki umeenea hadi baharini. Vizimbi vikubwa vinatengenezwa kwa seng'enge na kuzamishwa katika sehemu ya bahari pasipo hatari ya mawimbi makali kwa mfano katika hori nyembamba kama fyord za Norwei.
 
Back
Top Bottom