Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mtandao huo utatumiwa na mitambo ya kupeleleza anga za juu kutuma picha, video na maelezo hadi duniani.
"Tunatuma mitambo hii miwili kwenye Mwezi na tutakusanya data, video za HD na picha nyingi zenye maelezo na umuhumu kisayansi. Tatizo ni kwamba hatuwezi kuzituma moja kwa moja kutoka kwa mitambo hiyo hadi duniani. Hii ni kwa sababu itatumia nishati nyingi," amesema Kate Arkles Gray wa shirika la PTScientists.
 
Kwa hivyo, kutumia mtandao wa 4G kwenye Mwezi kutatuwezesha kutuma data, video na picha hizo hadi kwenye mtambo wa kutua kwenye Mwezi ambao una nishati nyingi, na unaweza basi kuvituma hadi duniani."
"Kwa kufanya hivyo, tutaweza hata kuzitazama video hizo za HD moja kwa moja kutoka kwenye Mwezi tukiwa hapa duniani.
 
Naam, ni kweli naegemea upande mmoja kwa sababu mimi hufanyia kazi kampuni inayoangazia upelelezi wa anga za juu lakini kuna mambo na vitu vingi sana ambavyo tunavitumia kwa sasa duniani kila siku ambavyo vilianza kama teknolojia ya kutumiwa anga za juu," anasema Bi Gray.
 
Back
Top Bottom