Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

2. Kupanda kwa mstari
Upandaji wa mbegu kwa mstari unatakiwa kutengeneza mifereji inayo katisha upana wa tuta kwa kutumia kijiti. Mfereji huu uwe na kina kisichozidi sm 2 hadi sm 3. Kupanda mbegu ndogo ndogo kama vile vitunguu, nyanya na kabichi tumia mifereji yenye kina cha sm 2 ili huepusha kuoza kwa mbegu kama zikipandwa chini sana. Weka umbali wa sm 15 hadi 20 kati ya mstari na mstari. Baada ya kupanda mbegu katika mstari rudishia udongo na baadaye shindilia udongo ili uweze kushikana na mbegu vizuri.
 
Mbegu zikishafunikwa kwa udongo, tandaza nyasi juu ya tuta la kitalu ili kuzuia maji kupotea hewani na kukauka kwa tuta na mbegu kabla na baada ya kuota. Kisha mwagilia maji kiasi na baada ya hapo tuta limwagiliwe maji asubuhi na jioni kulingana na hali ya hewa na aina ya udongo. Unaweza kumwagilia maji hadi mara tatu kwa siku kwa sehemu zilizo na jua kali au udongo wa kichanga.
 
Matunzo ya kitalu
Ondoa nyasi juu ya kitalu mbegu zikishaota. Jengea kichanja kilichotandazwa nyasi au makuti ama kitu chochote ili punguza kupenya kwa mionzi ya jua kwa sababu miche hii bado ni michanga sana hivyo huathirika kwa jua kali ambalo linaweza kuiunguza au kuifanya isikue vizuri. Kichanja kiki kiwe na urefu wa mita moja ili kuwezesha ung’oaji wa magugu na kupunguzia miche bila tatizo lolote.
 
Kichanja hupunguza kasi ya matone ya mvua kubwa ambayo inaweza kujeruhi miche michanga. Kichanja cha kitalu kinaweza kukaa kwa muda wa wiki mbili. Punguza kiasi cha kivuli cha matandazo ya nyasi pole pole na unaweza kutoa kabisa baada ya wiki mbili au tatu.
Miche yenye majani mapana kama vile, kabichi na nyanya, inahitaji kupunguziwa ili kutoa nafasi ya kukua vizuri. Miche ihamishwe mapema maana kuhamisha miche mikubwa ni vigumu zaidi kwa sababu mizizi yake ni mirefu na inaweza kukatika kirahisi.
 
Utayarishaji wa miche ya kupanda shambani
Ondoa kivuli baada ya wiki mbili au tatu tangu kuota kwa miche ili husaidia miche ianze kuzoea hali halisi ya bustanini hasa jua na upepo mkali. Wiki moja kabla ya kupeleka miche bustanini yaani baada ya wiki
nne kwa mazao mengi ya mboga (kasoro kitunguu wiki 5) punguza kiwango cha maji ya kumwagilia ili miche izoee hali ngumu ya ukame baada ya kupandikizwa bustanini. Miche ipandikizwe ikiwa na udongo kidogo kuzunnguka mizizi yake ili iweze kushika vizuri mara baada ya kupandikizwa shambani.
 
UTHIBITI WA MAGONJWA NA WADUDU KATIKA MBOGA
Wadudu na magonjwa hupunguza kiasi cha mavuno na hata kuua mimea kabisa, Hupunguza ubora wa mboga, Huongeza gharama za uzalishaji, hasa madawa ya viwandani yanapotumiwa na Huongeza uharibifu wa mboga baada ya kuvuna.
Ni lazima utambue aina ya ugonjwa au mdudu ili utumie kinga Ianayostahili kukabili. Ili kufanikisha lengo hili unaweza kutumia uzoefu wako, hasa baada ya kuwa na wataalam wa wadudu na magonjwa ya mimiea kwa muda mrefu, Kutumia mabwana shamba, Kutumia wataalam wa magonjwa na wadudu wa mboga au kuchunguza sehemu ya mmea uliyougua kwenye maabara.
 
Kanuni za kukinga mboga dhidi ya magonjwa na wadudu
Panda mazao muda unaotakiwa hii itakuwezesha kukwepa baadhi ya magonjwa ya msimu.
Usipande mboga ya jamii moja katika eneo moja kwa misimu mingi mfululizo. Changanya mazao au mimea ambayo inafukuza magonjwa na wadudu kama vile mimea inukayo
Chagua udongo usiokuwa na magonjwa ya mboga unayotaka kuzalisha.
 
Tumia mbegu bora, kwani baadhi ya magonjwa hutokana na mbegu.
Hakiksha kuwa vitalu, bustani na sehemu ya kuhifadhi mboga ni safi kwani uchafu na magugu huvutia magonjwa na wadudu waharibifu.
Hakikisha unatoa majani au mimea iliyokwisha ugua, na ichome moto au ifukie..
Usichanganye mboga na baadhi ya mazao yanayovutia magonjwa au wadudu katika bustani yako. Mfano mazao kama mipapai na bamia huvutia nzi wadogo weupe wanaoeneza ugonjwa wa "ukoma wa nyanya".
Tumia madawa ya asili na viwandani ili kupunguza kuenea kwa magonjwa na wadudu. Unalazimika kukinga mboga dhidi ya magonjwa na wadudu kwa kutumia madawa ya asili na viwandani pale mbinu nyingine zinaposhindwa kuleta mafanikio.
 
4B9914D8-9204-4C80-B881-6E3B0BBB8FD5.jpeg
 
Usipige dawa wakati wa mvua (mara tu kabla ya mvua) kwani maji ya mvua yataosha na kupunguza nguvu ya dawa.
Unashauriwa kupiga dawa wakati wa asubuhi hasa kukinga magonjwa ya ukungu yapendayo unyevunyevu. Kwa kuzuia wadudu, ni vizuri kupiga dawa wakati wa jioni. Wakati wa jioni dawa huua wadudu zaidi kwani hukaa muda mrefu juu ya majani kabla ya nguvu yake kuharibiwa na jua.
 
Weka kiwango cha dawa kama ilivyo elekezwa na watengenezaji au watalaam. Kiasi kidogo cha dawa katika maji hufanya viini vya magonjwa na wadudu kuwa sugu.
Kumbuka kuwa kiasi cha sumu ndani ya kasha au kopo la dawa hutofautiana kati ya kampuni na kampuni iliyotengeneza.
Ikiwezekana tafuta ushauri kwa muuza madawa au wataalam waliokaribu nawe.
 
Hakikisha unapiga dawa ya kutosha sehemu zote za mmea kwani baadhi ya wadudu au magonjwa hukaa na kushambulia sehemu ya chini ya majani.
Andaa vizuri bomba la kupigia dawa kabla ya kuchanaganya dawa na maji ili dawa iweze kutoka vizuri.
Madawa hutofautiana sana nguvu za kuua wadudu, hivyo changua madawa yanayofaa kufuatana na ugonjwa na wadudu.
 
Unashauriwa kupiga madawa hasa ya viwandani siku 14 kabla ya kuvuna mboga Pamoja na kuepuka kupiga madawa mara kwa mara kwa usalama wa mlaji.
Epuka Kupiga dawa ya aina moja mara kwa mara dhidi ya ugonjwa au mdudu wa aina moja kwa sababu hii kufanya hivyo huwafanya wadudu kujenga sugu dhidi ya dawa hiyo.
 
Madawa ya asili
Madawa ya asili ni mengi ila bado hajafanyiwa utafiti wa kutosha kuhusu aina ya wadudu na magonjwa ninayotibu, jinsi ya kutumia na kiasi cha kutumia. Baadhi ya mimiea inayotoa madawa ya asili ni mbegu na majani ya muarobaini, tumbaku, pilipili kali, pareto, kitunguu swaumu, manung'anung'a, n.k. Muarobaini ni miongoni mwa mimea michahce ambayo mpaka sasa imefanyiwa utafiti wa kiina. Mfano, kuchanganya nusu kilo ya mbegu za muarobaini zilizotwangwa katika lita ishirini za maji husaidia kuua wadudu mbalimbali wakiwemo funza wanaotoboa matunda ya nyanya.
 
Madawa ya asili ni bora zaidi kuliko madawa ya viwandani kwani sumu yake ni kidogo na hupungua haraka baada ya kupiga dawa. Hivyo ni salama zaidi kwa mpigaji dawa na mlaji mboga. Hivyo kupendekezwa katika kilimo hai na hifadhi ya mazingira.
 
Kasoro kubwa katika kutumia madawa ya asili ni kwamba hayajafanyiwa utafiti wa kutosha ukilinganisha na yale ya viwandani. Mfano, nitumie dawa ipi inayofaa kwa mdudu yupi?. Nguvu yake ni kidogo, hayatafaa kuzuia mashambulizi makubwa ya magonjwa au wadudu vilevile yanakinga zaidi mboga dhidi ya wadudu waharibifu kuliko magonjwa.Pia uwiano wa kuchanganya dawa na maji bado haujulikani vizuri. Mfano, niweke kiasi gani cha dawa katika kiasi gani cha maji ?..
 
Madawa ya viwandani
Madawa ya viwandani yana sumu nyingi zaidi na hivyo huzuia haraka zaidi mashambulio ya magonjwa na wadudu. Hivyo, hutumika sana katika kilimo cha mboga na mazao mbali mbali kuliko madawa ya kienyeji. Changamoto la haya madawa ni kwamba ni hatari kwa mkulima, mlaji wa mboga, mazingira na pia gharama zake ni kubwa.
 
KUVUNA NA KUHIFADHI MBOGA
Uvunaji wa mboga
Uvunaji wa mazao ya mboga ni hatua ya mwisho na muhimu sana katika uzalishaji. Kabla ya kuchukua uamuzi wa kuvuna mboga ni muhimu kufanya utafiti wa soko la mavuno hayo, kutafakari na kuchagua aina au njia ya kuvuna na kusafirisha mazao hadi kwenye soko. Ni muhimu kupanga mipango hii mapema ili pindi zao linapokomaa uvunaji ufanyike na hivyo kuepuka zao kubakia bustanini kwa muda mrefu ambao utasababisha kuharibika.
 
Unapaswa kuwa makini sana katika mipangilio ya shughuli zake ili kujipatia mavuno mengi na bora na baadaye kuweza kuyauza kwa bei nzuri.

Jinsi ya kutambua ukomavu unaofaa kwa kuvuna mboga za aina mbali mbali.
Dalili au kipindi cha ukomavu unaofaa kwa kuvuna mboga maranyingi hutokana na uzoefu wa mkulima mwenyewe pamoja na mahitaji ya soko, umbali wa kusafirisha mboga na aina ya usafiri utakao tumika kusafirisha mboga. Kumbuka kuwa mboga ni mazao yasiyoweza kuhifadhika kwa muda mrefu na yanahitaji kutumiwa haraka mara tu baada ya kuvunwa.
 
Back
Top Bottom