Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Buibui na ng’e

Ingawa wanaweza kusababisha maumivu makali, matukio mengi ya kuumwa na buibui na ng’e hayasababishi madhara makubwa au madhara ya muda mrefu. Usiitikise sehemu iliyoumia na tumia barafu au maji baridi kupunguza maumivu.Usikate au kuchana wazi sehemu ya jeraha au kufunga sehemu hiyo kwa kutumia toniketi au bandeji. Joto halisaidii, lakini kutoitikisa sehemu ya jeraha husaidia.
 
Kwa ajili ya matukio ya kunga’twa na buibui na ng’e hatari, unaweza kumpa majeruhi diazipamu kuzuia misuli kukakamaa na pia kumtuliza mgonjwa wakati mnafanya maandalizi ya kwenda hospitali au kituo cha afya.
 
Nyuki na nyigu
Baada ya kuumwa na nyuki, angalia kama mwiba wake umebaki kwenye ngozi na kuuondoa haraka iwezekanavyo. Eneo inayozunguka sehemu ya jeraha inaweza kuwa na wekundu, kuvimba na kutoa maumivu. Kuweka mgando wa amira na maji, au kitu kingine baridi kwenye eneo husika, kutasaidia kudhibiti uvimbe na maumivu
 
Nyuki na nyigu
Baada ya kuumwa na nyuki, angalia kama mwiba wake umebaki kwenye ngozi na kuuondoa haraka iwezekanavyo. Eneo inayozunguka sehemu ya jeraha inaweza kuwa na wekundu, kuvimba na kutoa maumivu. Kuweka mgando wa amira na maji, au kitu kingine baridi kwenye eneo husika, kutasaidia kudhibiti uvimbe na maumivu
 
Samaki na Yavuyavu (jelly fish)
Jinasue kutoka kwa yavuyavu na kwangua miguu yake ambayo inaweza kuwa imekung’ang’ania. Tumia maji ya bahari kunawa sehemu hiyo. Kwa samaki wanaochoma na miba yao, ondoa miba yote iliyobaki kwenye ngozi kwa kutumia kibanio.
 
Ingiza sehemu iliyoumia kwenye maji ya moto kwa dakika 20 kupunguza maumivu, lakini hakikisha kuwa hayaunguzi. Hii inaweza kusaidia zaidi kutuliza majeraha kutokana na samaki wanaochoma kuliko yavuyavu.
 
Kuna tiba nyingi za asili lakini siyo zote hufanya kazi dhidi ya madhara ya aina zote za samaki au yavuyavu. Kwa mfano, mashambulizi ya samaki wengine yanaweza kutulizwa kwa kuosha na siki (vinegar). Lakini siki huzidisha madhara ya mashambulio ya aina zingine za yavuyavu. Papai au vilainisha nyama ni vitulizo muhimu v ya maumivu kutokana na mashambulizi ya yavuyavu,. Papai au vilainisha nyama ni vitulizo muhimu vya maumivu kutokana na mashambulizi ya yavuyavu, lakini siyo kwa aina zote za yavuyavu na wakati mwingine vinaweza kuzidisha maumivu.
Mhimize atumie na kutembeza viungo vyake —tofauti na matukio ya kung’atwa na nyoka au buibui, kutuliza kiungo bila mtikisiko hakusaidii. Tafuta msaada wa kitabibu kama kutakuwa na matatizo ya kupumua au iwapo dalili zitazidi kuwa mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…