Mfano mwingine wa kazi ya nguvumaji ni buibui inayoruka, ambapo damu iliyolazimishwa kuelekea kwenye miguu chini ya shinikizo husababisha inyooke kwa nguvu na hivyo kuifanya iruke, bila haja ya kuwa na miguu minene yenye misuli. [2
Kati ya wadudu, damu (ambayo inaitwa vizuri zaidi hemolimfu) haihusishwi katika usafirishaji wa oksijeni (mianya inayoitwa bomba za pumzi huruhusu oksijeni kutoka kwa hewa kuenea moja kwa moja hadi kwenye tishu). Damu ya wadudu husafirisha virutubisho hadi kwenye tishu na huondoa bidhaa taka katika mfumo wazi.
Wanyama wengine wasio na uti wa mgongo hutumia protini za kupumua ili kuongeza uwezo wa kubeba oksijeni. Himoglobini ndiyo protini ya kupumua inayopatkana sana katika mazingira asili. Himosianini (buluu) ina shaba na inapatikana katika krasteshia na moluska.
Inadhaniwa kwamba tuniketi (mnyama wa baharini anayetoa maji kupitia tundu mbili anapoguswa) anaweza kutumia vanabini (protini zenye vanadiamu) kwa pigmenti ya kupumua (kijani-ng'avu, buluu, au rangi ya machungwa).
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.