Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kati ya wanyama wengi wasio na uti wa mgongo, protini hizi za kubeba oksijeni huyeyuka kwa urahisi katika damu; kati ya wanyama wenye uti wa mgongo zinapatikana katika seli maalumu nyekundu za damu, zinazoruhusu ukolezi wa juu zaidi wa pigmenti za kupumua bila kuongeza mnato au kuharibu viungo vinavyochuja damu kama vile figo.
 
Minyoo wakubwa huwa na himoglobini zisizo za kawaida zinazowaruhusu kuishi katika mazingira yasiyo ya kawaida. Himoglobini hizi pia hubeba salfaidi ambazo kwa kawaida ni hatari kwa wanyama wengine.
 
Himoglobini ndiyo chanzo kikuu cha rangi ya damu katika wanyama wenye uti wa mgongo. Kila molekuli ina makundi manne ya heme, na mwingiliano wao na molekuli mbalimbali hubadili rangi halisi. Kati ya wanyama wenye uti wa mgongo na viumbe vingine vinavyotumia himoglobini
 
damu ya ateri na damu kutoka kwa mishipa ni mwekundu wenye kung'aa, kwa kuwa oksijeni huipa kikundi cha heme rangi nyekundu iliyokoza. Damu isiyo na oksijeni huwa ni nyekundu iliyokoza zaidi; hii inapatikana katika vena, na inaweza kuonekana wakati wa uchangiaji wa damu na wakati sampuli za damu kutoka kwa vena zinapochukuliwa.
 
Damu iliyopata yenye sumu ya monoksidi ya kaboni ni nyekundu inayoyong'aa, kwa sababu monoksidi ya kaboni husababisha uundaji wa kaboksihimoglobini. Katika sumu ya sianidi, mwili haiwezi kutumia oksijeni, kwa hivyo damu ya vena bado hubaki ikiwa na oksijeni na hivyo kuongeza wekundu.
 
Ingawa damu yenye himoglobini kamwe haiwi na rangi ya buluu, kuna hali kadhaa na magonjwa ambapo rangi ya makundi ya heme hufanya ngozi ionekane ikiwa na rangi ya buluu. Ikiwa heme imewekewa oksijeni, methimoglobini, ambayo ni ya kahawia zaidi na haiwezi kusafirisha oksijeni, inaundwa. Katika hali isiyo ya kawaida ya salfahemoglobinemia, sehemu ya himoglobini ya ateri huwekwa oksijeni, na huonekana kuwa na rangi nyekundu iliyokoza na rangi ya bluu (sainosisi).
 
Vena katika ngozi huonekana kuwa na rangi ya bluu kutokana na sababu mbalimbali ambazo hutegemea rangi ya damu kwa kiwango kidogo pekee. Kujitokeza kwa sehemu nyeupe kwenye ngozi na uchakataji maono ya rangi pia huchangia. [
 
Damu ya moluska wengi - ikiwa ni pamoja na sefalopodi na gastropodi - pamoja na baadhi ya wadudu, kama vile kaa aina ya Horseshoe, yenye rangi ya buluu, kwa kuwa ina protini za himosianini zenye ukolezi wa kama gramu 50 kwa lita.
 
Himosianini huwa haina rangi wakati haina oksijeni na ni buluu iliyokoza wakati inapoongezewa oksijeni. Damu inayozunguka ndani ya viumbe hawa, ambao kwa ujumla huishi katika mazingira baridi yenye mivuto ya chini ya oksijeni, huwa ni rangi ya kijivu-nyeupe hadi manjano hafifu,
 
na hugeuka kuwa buluu iliyokoza wakati inapoachwa wazi kwa oksijeni iliyo kwenye hewa, kama ilivyo wakati vinatoka damu. [25] Hii ni kutokana na mabadiliko ya rangi ya himosianini wakati inapoongezewa oksijeni. [25] Himosianini hubeba oksijeni katika giligili iliyo nje ya seli, ambayo ni tofauti na usafirishaji wa oksijeni ndani ya seli kwa mamalia kupitia himolobini katika RBC. [25]
 
Matatizo ya kiwango
Jeraha linaweza kusababisha upotezaji wa damu kupitia kutoka damu. [26] Mtu mzima mwenye afya anaweza kupoteza karibu 20% ya kiasi cha damu (1 L) kabla ya dalili ya kwanza, kutotulia, kuanza, na 40% ya kiasi cha damu(2 L) kabla ya mshtuko. Thrombosaiti ni muhimu kwa ugandishaji na uundaji wa madonge ya damu, ambayo inaweza kusimamisha upotezaji wa damu. Majeraha mabaya kwa viungo vya ndani au kwa mifupa yanaweza kusababisha kutokwa na damu kwa ndani, ambayo wakati mwingine unaweza kuwa kali.
 
Kuishiwa maji mwilini kunaweza kupunguza kiasi cha damu kwa kupunguza kiwango cha katika damu. Mara nadra, hii inaweza kusababisha mshtuko (isipokuwa katika kesi kali sana) lakini huweza kusababisha kupungua kwa shinikizo la damu kunakosababishwa na kusimama na kuzirai.
 
Matatizo ya mzunguko
Mshtuko ni upiliziaji usio bora wa tishu, na unaweza kusababishwa na hali mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupoteza damu, maambukizi, kupunguka kwa uwezo wa moyo wa kusukuma damu.
 
Back
Top Bottom