Sis, jana kwa bahati tu nikafungua TV kuangalia kipindi changu nikipendacho sana cha Ancient Aliens mara paaap kumbe wanamwongelea Malkia Isis. Basi nikasogeza daftari na kalamu kabisa. Nilijifunza mengi. Kimsingi walikuwa wanadai kwamba inawezekana kuwa ISIS na miungu wenzake wa kale si miungu tu bali yawezekana Wamisri waliwaabudu kwa sababu miungu hiyo ilitoka huko mbali katika sayari zingine na ndiyo iliyowafundisha teknolojia ya kushangaza. Jamaa wako deep sana na kuna maprofesa, wanahistoria, wanasaikolojia, wanathiolojia na wanasayansi ambao maisha yao yote wameshughulika na haya mambo. Duniani hapa kuna vitu vingi sana ambavyo hatuvijui na elimu tunayofundishwa mashuleni imechujwa kwa uangalifu mno...