Umoja wa madereva wanaosafirisha magari nje ya nchi (ITDA) wameiomba Serikali kufikiria kutunga sheria ndogo ili kulinda ajira za wazawa kufuatia kazi nyingi kuchukuliwa na wageni.
Kilio hicho kimetolewa leo Machi 10, 2018 wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa umoja huo ambao ulilenga kujadili masuala mbalimbali ikiwemo uhakika wa ajira zao.
Amesema hali hiyo imekuwa kikwazo kikubwa cha ajira kwa wazawa ambao wamekuwa wakitegemea kupata kazi za kusafirisha magari hayo na hivyo kujiongezea kipato.
"Hali imekuwa mbaya bandari yetu lakini tunaishia kuangalia maji, wenzetu kazi wanapeana wenyewe kwa wenyewe, ukifuatilia kwa undani madereva wengi sasa hawana kazi," amesema Mhina.

Mwenyekiti wa ITDA, Jimmy Mwalugelo amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kueleza kuwa jitihada zinaendelea kufanyika kupata ufumbuzi.
Amesema hali hiyo ni matokeo ya makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki hivyo ni muhimu kuheshimu makubaliano hayo.
Amesema ili kupata ufumbuzi ni muhimu Serikali ikaanzisha sheria ndogo itakayoelekeza magari yote yanayotoka bandarini yaendeshwe na dereva aliyepitia mafunzo maalum yatakayotolewa katika Chuo cha Muhonda.

Tunafanya utaratibu wa kuanzisha chuo, ambacho kitakuwa kinatoa mafunzo mafupi na yenye tija kwa madereva wanaokwenda nje ya nchi, hawa tutawapatia vyeti,"amesema.
Ndiyo sababu tunashauri kwa kusaidia kulinda ajira za wazawa iwekwe sheria itakayomtaka dereva anayetoa gari bandarini awe na cheti hiki pamoja na leseni."
Ndiyo sababu tunashauri kwa kusaidia kulinda ajira za wazawa iwekwe sheria itakayomtaka dereva anayetoa gari bandarini awe na cheti hiki pamoja na leseni."
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.