Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

TATIZO LA MAWE KWENYE FIGO(KIDNEY STONES)
-Figo ni kiungo muhimu katika mwili wa binadamu,hufanya kazi ya kuchuja damu huku ikiondoa sumu zote za mwili,figo hufanya kazi ya kurekebisha kiasi cha maji mwilini(electrolyte level).
kabla damu haijapita katika figo,huwa imebeba maji na takataka nyingi sana(urea)
 
,lakini inapopita katika figo huchujwa na vitu muhimu hurudishwa katika mzunguko wa damu lakini,masalia mengine ambayo hayafai tena katika mwili ikiwa ni pamoja na kiwango cha maji kilichozidi hupitishwa kwenye mirija miwili(ureters)kuelekea kwenye kibofu(urinary bladder) na kishas kutolewa nje ya mwili kupitia njia ya mkojo(urethra)
 
Mkusanyiko wa kemikali hizi(chemical crystals),wakati mwingine hugandamana na kutengeneza chembechembe ya vitu kama mchanga,kadri siku zinavyozidi kuendelea ndivyo vinavyozidi kukua hadi wengine hufikia hatua ya kuziba njia ya mkojo katika figo yenyewe(neprone) au kwenye mirija ya kupeleka mkojo kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu(ureteter),hapo ndipo mtu anaanza kupata shida ya kukojoa na kusikia maumivu makali.
 
DALILI ZA UWEPO WA MAWE KWENYE FIGO;
Mtu mwenye mawe kwenye figo huonyesha dalili zifuatazo;
a.Maumivu ya mgongo na kiuno
b.Mkojo kutoka ukiwa na rangi ya damu
 
c.Kutokwa na jasho wakati wa usiku
d.Kupatwa na homa kali kwa wakati flani ikiambatana na kutetemeka mwili
 
h.Miguu kujaa maji/kuvimba.
i.Maumivu ya tumbo chini ya kitovu upande wa kushoto au kulia kutegemea ni figo ya upande gani iliyoathirika.
j.Maumivu makali unapogusa upande wa figo iliyoathirika.
 
Back
Top Bottom