Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nasema hivyo kwa sababu matumizi ya dawa kiholela yanaweza kusababisha sumu mwilini, kwani mtu anapozitumia bila vipimo na ushauri kutoka kwa daktari, anaweza kukosea chaguo na kumeza ambazo hazihusiani na ugonjwa anaougua.
 
moto uliteketeza soko lote la Mbagala Rangitatu lililokuwa na vibanda vya wafanyabiashara 673.

Janga hilo ambalo imedaiwa kusababishwa na hitilafu ya umeme, limetokea siku mbili tu tangu bweni la Sekondari ya Wasichana Korogwe nalo kuteketea kwa moto.
 
Lakini tatizo tunaloliona ni elimu duni au uelewa mdogo juu ya namna ya kujikinga na majanga ya moto ambayo tunaamini kwamba Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likijipanga na kuweka mikakati, balaa hili linaweza kudhibitiwa kwa kiwango kikubwa.
 
Tunatarajia kwamba kutokana na matukio ya aina hiyo kuwa mengi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wangekuja na mikakati ya mafunzo kwa wananchi hasa wale wanaofanya shughuli zao kwenye mikusanyiko mikubwa juu ya matumizi bora ya mfumo na salama wa umeme ili kuokoa maisha na mali zao pindi tatizo kama hilo linapojitokeza.
 
Watu hawa wanahitaji kuelimishwa kuhusu matumizi sahihi ya vifaa vya umeme kwenye nyumba na maeneo yao ya biashara. Majanga mengine yamekuwa yakisababishwa na ujuvi wa masuala ya umeme na kufikia hata kuhamisha nyaya bila kuzingatia weledi na vifaa stahiki.
 
Pia wakati mwingine moto unatokana na hitilafu ya umeme husambaa na kusababisha madhara makubwa kutokana na kuhamaki au kutojua kwamba unapotilia shaka au inapotokea moto wa aina yoyote katika nyumba, jambo la kwanza ni kukimbia kwenye swichi kuu (main switch) na kuizima.
 
Tunaamini kabisa kwamba elimu ya majanga ikiyafikia makundi makubwa ya watu kama wafanyabiashara katika masoko, wanafunzi, viwandani na taasisi zenye mikusanyiko mikubwa ya watu, siyo tu itazuia majanga hayo katika maeneo hayo, bali itasambaa kwani watakaoelimishwa nao watafanya hivyo katika nyumba zao na watawaelimisha ndugu jamaa na marafiki.
 
Hivyo, ni jukumu la kila mmoja wetu kujisaili kama mahali anapofanyia kazi au anapoishi ni salama na amechukua kila aina ya tahadhari ya majanga hasa ya moto. Pamoja na hayo, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiamua, wakawezeshwa, miaka ijayo tutashuhudia takwimu za mabalaa haya zikishuka.
 
Licha ya kuwapo hasama ya kukuza viwanda nchini, Kiwanda cha Sukari cha Zanzibar kimenyimwa kibali cha kuuza zaidi ya tani 3,000 ya bidhaa hiyo upande wa bara.

Meneja biashara wa kiwanda hicho, Pranav Shah alisema wameshindwa kuuza sukari hiyo Zanzibar kwa sababu wanapata hasara ya Sh18,000 kwa kila mfuko wa kilo 50 wakitoa gharama za uzalishaji.
 
Tunataka soko la bara kwa sababu ya tofauti ya bei iliyopo. Hapa tunauza mfuko wa kilo 50 kwa Sh65,000 hadi Sh70,000 wakati Dar es Salaam inauzwa Sh115,000.

“Tunazo tani 3,000 tulizozalisha tangu Januari, tumeshindwa kuuza kuepuka hasara. Kuuza bara tunahitaji kibali ambacho hatujapata mpaka sasa,” alisema Shah.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…