Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hili nimelishuhudia mara nyingi pale mtu anapohisi dalili za ugonjwa fulani bila ya kuwa na uhakika, hukimbilia dukani kununua dawa na kuzitumia.
 
Hili nimelishuhudia mara nyingi pale mtu anapohisi dalili za ugonjwa fulani bila ya kuwa na uhakika, hukimbilia dukani kununua dawa na kuzitumia.
 
Yaani kama mtu aliugua malaria mara moja kisha akapata vipimo kutoka kwa daktari na kupewa dawa akapona, hiyo kwake inatosha. Anakariri na kujijengea imani kuwa atakapokuwa na dalili kama hizo tena, moja kwa moja anaamini ni malaria na huamua kununua dawa na kuzinywa bila ushauri kutoka kwa daktari.
 
Kuna muuza duka mmoja aliwahi kuniambia, “Wanaokuja kununua dawa bila kuwa na cheti kinachoonyesha vipimo kutoka kwa daktari huwa nawashauri waende hospitali kwanza wakapime, ila kuna tatizo kubwa, mtu anakwambia we nipe tu dawa mimi ndiyo ninayeumwa na najua ninachoumwa wewe nipe dawa ninazotaka.”
 
Lakini pia kuna baadhi ya maradhi hasa ya zinaa ambayo humfanya mtu aone aibu kwenda hospitali na kuamua kununua dawa na kuzitumia bila vipimo na matokeo yake anaweza akajikuta ndiyo anachochea kasi ya ugonjwa.
 
Ili kudhibiti hali hiyo, kuna haja sasa kwa Serikali na wadau wa afya nchini kutoa elimu ya kina ili watu waachane na tabia hiyo ambayo ni hatari kwa afya zao.
 
Back
Top Bottom