Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Dawasco pia, imejipanga kuongeza mtandao wa usambazaji maji kwa mwaka wa fedha 2018/19 na kwamba Sh62 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.

Mhandisi Luhemeja amesema upanuzi huo umelenga kuyafikia maeneo ya Tabata,Temeke, Kigamboni, Kimara na kwenye viwanda wilayani Kibaha.
 
Vilio, simanzi na majonzi vimetawala kwa waombolezaji kutoka jijini Mwanza na maeneo jirani wanaendelea na ibada ya mazishi ya mfanyabiashara Samson Josia yanayofanyika nyumbani kwake mtaa wa majengo mapya wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

Mwili wa mfanyabiashara huyo uliokutwa ukiwa umefungwa kwenye viroba ukielea ndani ya Mto Ndabaka mpakani mwa wilaya za Bunda mkoa wa Mara na Busega mkoani Simiyu umewasili asubuhi ya leo Machi 16 ukitokea Hospitali ya Rufaa Mara ulikohifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi tangu juzi.
 
Tangu asubuhi, mamia ya waombolezaji kutoka jijini Mwanza na maeneo jirani wamekuwa wakimiminika nyumbani kwa marehemu wakitumia mabasi ya kampuni aliyokuwa akimiliki.

Mabasi ya kampuni nyingine pia yanatumika kusafirisha waombolezaji kutoka jijini Mwanza bila malipo
 
Marehemu Josia aliyezaliwa mwaka 1968 alipotea tangu Februari 27 kabla ya gari lake kukutwa likiwa limeteketezwa kwa moto ndani ya eneo la hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara Machi 9.

Ibada ya mazishi inaongozwa na Mchungaji Jackson Meza kutoka Kanisa la African Inland Church of Tanzania (AICT) huku kwaya ya kanisa ambayo marehemu alikuwa mfadhili wake ikiimba nyimbo za maombolezo.
 
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Jaffari Mohamed, watu wanne wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano kuhusiana na kifo hicho kilichoibua hofu na maswali yasiyo na majibu miongoni mwa ndugu, jamaa, marafiki na wakazi wa jiji la Mwanza ambako marehemu alikuwa akiendesha shughuli zake za kibiashara.
 
.Mwili wa mfanyabiashara wa mabasi ya Super Sam umewasili nyumbani kwake mtaa wa majengo mapya wilayani Magu kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Mwili huo ulipatikana juzi ikiwa ni siku tano baada ya gari lake aina ya Toyota Land Cruiser kukutwa limeteketezwa kwa moto ndani ya eneo la hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Ijumaa iliyopita.
 
Mfanyabiashara huyo ambaye mabasi yake yanasafiri kati ya mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Iringa na Kagera alikuwa akiishi wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

Mfanyabiashara huyo alitoweka tangu Februari 27 ambayo ilikuwa siku ya mwisho kuwasiliana na familia yake.
 
Timu ya Liverpool imejikuta ikiangukia mdomoni mwa Manchester City kwenye droo ya hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Timu zingine ambazo zitakutana kwenye robo fainali hiyo ni Barcelona ambayo imepangwa na As Roma. Pia Sevilla wameangukia kwa Bayern Munich.
 
Droo hiyo iliyochezeshwa Ijumaa pia imezipanga pamoja Real Madrid na Juventus ambazo zimewahi kukutana hatua ya fainali mwaka 2017.
 
Makamu wa Rais wa Shirikisho Soka la Tanzania (TFF), Michael Wambura amefungiwa kutojihusisha na masuala ya soka maisha baada ya kukutwa na hatia,na Kamati ya Maadili ya TFF iliyokutana jana na kufikia hatua hiyo.
 
Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema kamati hiyo iliyokaa jana ikiongozwa na Mwenyekiti wake Hamidu Ally Mbwezereni, wamemkuta na makosa matatu yatakayomfanya Wambura asijihusishe na masuala ya soka.
 
Kosa la kwanza amevunja kifungu no 73 kwa kupokea malipo yasiyo halali ya TFF, ambapo faini yake ni milioni 10, kutojihusisha na soka miaka mitano au maisha.
 
Kosa la pili kugushi malipo kwa jina la TFF enzi hizo (FAT), ambapo amezuiliwa kujihusisha na soka kwa miaka 5.
 
Kosa la tatu linalomkabili ni kushusha hadhi ya TFF, kosa ambalo adhabu yake iliyotolewa ni kutojihusisha na soka maisha.
 
Dawa ni tiba pale tu mgonjwa anapozitumia vizuri kwa kuzingatia maelekezo muhimu kutoka kwa wataalamu wa afya wakiwamo madaktari baada ya kufanyika kwa vipimo na uchunguzi kuhusiana na ugonjwa husika.
 
Zisipotumiwa vizuri kwa kufuata ushauri wa madaktari, zinaweza kuleta madhara makubwa katika mwili wa binadamu.
 
Kumekuwa na mazoea ya watu kutumia dawa kiholela pindi tu wanapohisi kuumwa pasipo kufanya vipimo wala kupata ushauri kutoka kwa daktari au mtaalamu wa afya.
 
Back
Top Bottom