Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

2016-10-26%2011.34.05%201369447163760151405_3662913405.jpg
 
MATENDO NI TIBA YA WOGA.

Hii ndio dawa pekee ya kutibu ugonjwa wa woga ndani yako. Pindi tunapotaka kufanya jambo fulani utakuta tunakabiliwa na woga. Woga ni kitu kibaya sana katika maisha yetu ya kila siku. Jiulize ni mambo gani umeshindwa kuyafanya kwa sababu ya woga.
 
Siku zote ukitaka kushinda jambo kwanza ondoa woga ndani yako. Na ili kufanikisha jambo lako jiulize ni kitu gani ufanye ili kukabiliana na woga uliopo ndani yako. Jibu utakalolipata litumie kukabiliana na adui huyo woga. Utakuwa umepata muarobaini wa mafanikio yako.
 
Weka mfumo mpya sasa wa maisha yako, utakaokupa mwanga sahihi katika maisha yako. Utakuwa umekutana na fursa nyingi katika maisha yako ila woga umekufunika na kuiteka akili yako. Sasa ni wakati wa kukataa hali hiyo na kuamua kutenda. Nyanyuka tutembee pamoja sasa.
 
Duh pole,siku hizi huwa naona bora kutegemea msaada wa familia kuliko marafiki.
Nilikuwa huko December/January. Marafiki wengi waligeuka busy ghafla. Uzuri na mimi nilikuwa sihitaji cho chote just kuonana na kujuliana hali lakini huwezi kumpata mtu hata wale ambao niliamini kuwa tuko in good terms kutokana na kusaidiana kwa muda mrefu. Na usirogwe ikitokea akawa kapata vihela au kacheo kakubwa kidogo, maweee! Hapo ndo hutamsikia kabisaaaa wakati huku mitandaoni ulishakaribishwa vizuri na kwa mbwembwe kubwa ikiwa ni pamoja na picha za nyumba mpya na maprado. Ubinadamu kwishnei !!!
 
Kweli kabisa, ila kuna muda nafasi ya marafiki pia inakuwa na umuhimu wake. Sema sasa ndo ubahatishe rafiki/marafiki wa kujua umuhimu wa urafiki.
Bahat mbaya sijawah bahatisha wa hivyo,wengine ni wale wakiwa na shida wanakutafuta mara utaona sms watsup unashangaa hee leo nimekumbukwa kumbe ana shida
 
Wakazi wa Dar es Salaam wametakiwa kuacha kulalamikia uhaba wa maji kwa kuwa huduma hiyo inapatikana kwa wingi katika sehemu kubwa ya jiji.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Majitaka (Dawasco), Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema hayo leo wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji.
 
Amesema kuna changamoto kubwa ya watu kutoomba maji licha ya kuwa maji ya Dawasco yanapatikana katika maeneo yao.

Mhandisi Luhemeja amesema kwa sasa Dawasco inazalisha lita milioni 502 kwa siku ambayo ni sawa na asilimia 92 ya maji yanayohitajika.
 
Maji yapo tena mengi sana na tunaendelea na juhudi kuhakikisha tunayafikia maeneo yote, nichukue fursa hii kuwaambia wakazi Dar na Pwani, maji yapo waje waombe," amesema Mhandisi Luhemeja na kuwataka viongozi wa Serikali za mitaa kuwawezeshe wananchi kuzifikia huduma za shirika hilo.

"Viongozi wa mitaa wawakusanye wananchi wanaotaka maji, waje kwetu hatulipishi gharama zozote mwanzoni, utapigiwa hesabu kisha utaunganishiwa maji halafu utalipa taratibu," amesema.
 
Katika hatua nyingine, Mhandisi Luhemeja amesema shirika hilo linatambua ufinyu wa mtandao wa maji taka na liko mbioni kutatua changamoto hiyo.

Amesema tayari Sh26 bilioni na kazi ya upanuzi wa mtandao huo itaanza.

"Lengo ni kuwasaidia wananchi hasa katika maeneo yanayokumbwa na magonjwa ya kipindupindu kama Tandale, Mwananyamala Kisiwani na Makumbusho," amesema.
 
Back
Top Bottom