Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Klabu ya wekundu wa msimbazi Simba imeyaaga rasmi mashindano ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kutoka sare ya 0 – 0 dhidi ya timu ya Al Masry katika mchezo uliyopigwa nchini Misri.
 
Klabu ya Tottenham imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya FA Cup kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1991 baada ya kuifunga Swansea kwa jumla ya mabao 3 – 0 mchezo uliyopigwa dimba la the Liberty hii leo siku ya Jumamosi.
 
Licha ya kukosekana kwa mshambuliaji hatari wa timu hiyo Harry Kane kufuatia majeraha yanayomkabili lakini wachezaji, Christian Eriksen na Erik Lamela waliweza kuisaidia timu hiyo kuchomoza na ushindi huo mnono.
 
Meneja wa Spurs, Mauricio Pochettino anatazamiwa kutwaa kikombe hicho kwa mara yake ya kwanza ndani ya kikosi hicho.

Kikosi cha Swansea: Nordfeldt (7), Naughton (5), Van der Hoor (6), Bartley (5), Mawson (6), Olsson (6), Ki (5), Carroll (5), Clucas (5), Dyer (5), Abraham (5).
 
Wachezaji waakiba: Roberts (n/a), Routledge (n/a), Narsingh (6).

Kikosi cha Tottenham: Vorm (7), Trippier (7), Sanchez (7), Vertonghen (7), Davies (7), Dier (7), Sissoko (7), Lamela (8), Eriksen (9), Lucas Moura (7), Son (8).

Wachezaji waakiba: Alli (n/a), Llorente (6).

Mchezaji bora wa mechi hiyo ni Christian Eriksen.
 
MAKOCHA ni viongozi wa wachezaji. Ndio bila wao, wachezaji wasingeweza kuwa na mbinu za kufika langoni mwa timu pinzani. Lazima awepo mtu mmoja nje wa kuwaelekeza.
 
Huyo ndiye kocha. Lazima aheshimike kutokana na mchangoi wake kwenye timu. Wachezaji wengi wanawakubali makocha kutokana na mbinu zao. Utasikia mchezaji fulani anataka kuhamia timu fulani kwa sababu tu ya kocha. Anakubali mbinu zake.
 
Hata hivyo, hapa tunawaangalia wanasoka wa Bongo. Hawa wanavutiwa zaidi na makocha wa Ulaya ambao hata hivyo, hawawafundishi lakini wanazikubali na kutumia mbinu zao ili kuweza kujiongezea ujuzi zaidi wanapokuwa kwenye majukumu yao.
 
Salum Telela ‘Master’

Kiungo wa zamani wa Yanga na sasa anaichezea Ndanda FC ya Mtwara amemtaja Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ana mbinu nyingi za kiufundi.
 
Guardiola ni kocha mwenye mbinu nyingi, unaona timu inaweza kubadilika uwanjani kutokana na mchezo husika, ni kocha ninayemkubali na kumfuatilia kwa ukaribu kwa kile anachokifanya kwenye ulimwengu wa soka,” anasema.
 
Iddy Mobby

Beki wa Mwadui FC amesema anamkubali Kocha Jurgen Klopp wa Liverpool, kutokana na jinsi anavyojua kuhamasisha timu yake, iwe imeshinda ama kufungwa. “Ni kocha wa aina yake kwa uhamasishaji wake, hata kama wachezaji walikata tamaa, wanapata nguvu, pia inaonyesha yupo vizuri kisaikolojia kutokukubali kushindwa mpaka dakika ya mwisho,” anasema.
 
Elias Maguli

Kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuachana na klabu ya Dhofar ya nchini Oman, yeye amemtaja Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ni mzuri kiufundi, pia anajiamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…