George Kavila
Ni kiungo mkabaji wa Kagera Sugar, amesema kama kuna kocha wa Ulaya anayemkubali basi ni Jose Mourinho wa Manchester United na alianza kumfuatilia tangu akiwa Porto, Chelsea na Inter Milan. Kitu pekee anachokipenda kwa kocha huyo ni namna ambavyo ana mbinu za kiushindani na kuwasoma wapinzani wake na anaweza akabadili mfumo ili mradi apate matokeo.