Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kunde ni zao ambalo linaweza kulimwa kwa ajili ya chakula na bishara ni zoa lenye kiasi kukubwa cha protini na majani yake yanaweza kutumika kama mboga za majani.Ni zao ambalo linatoa mavuno ya Kiasi cha kilogram 500 hadi 1500 kwa ekari.
 
HALI YA HEWA IFAAYO
Ni zao linalostahimili ukame, Kunde hukubari vizuri katika mwinuko wa mita 0 hadi 1500 kutoka usawa wa bahari.kunde huweza kulimwa katika maeneo yapatayo mvua kidogo kiasi cha milimita 500 hadi 1200 kwa mwaka.Hukuwa vizuri katika joto la nyuzi 28 had 32 C.
 
3.ARDHI IFAAYO KWA KILIMO CHA KUNDE
Huweza kulimwa katika udongo usiotuamisha maji wa aina tofauti tofauti kuanzia kichanga hadi mfinyazi.Zinaweza kupandwa katika udongo usio na rutuba ya kutosha lakini hustawi vizuri katika udongo wa tifutifu kichanga au tifutifu mfinyanzi au mchanganyiko wa mfinyazi na kichanga wenye p.H kati ya 6 hadi 7
 
.MAANDALIZI YA SHAMBA LA KUPANDA KUNDE
Shamba la kunde liandaliwe mapema kabla shughuli ya upandaji kuanza, Kama ni la kukata miti mikubwa miti ikatwe mapema,Kama ni la kufyeka nyasi na miti midogo shughuli hii ifanyike mapema kabla hatua ya kulimwa kwa shamba kwa kutumia trekta,Pawatilla,jembe la ng'ombe au la mikono.shamba lisawazishwe na kukusanywa mabaki ya mimea au visiki na mawe madogomadogo kama yapo.
 
BAADHI YA MBEGU BORA NA SIFA ZAKE
1.TUMAINI

Hukomaa kwa muda wa siku 75 – 90. Aina hii ya kunde husambaa ina maua yenye rangi za zambarau na mbegu zake ni mviringo. Maeneo yanayoshauriwa kupanda ni yenye mwinuko wa mita 0 – 1500 toka usawa wa bahari. Inahitaji udongo mwepesi wenye rutuba na usiotuamisha maji. Kunde hizi hutoa mazao hadi tani 3 (kilogram 600 - 1500 kwa ekari)kwa hekta moja. Huvumilia virusi vya mozaiki vinavyotokana na wadudu mafuta wa kunde na bakiteria. Aina hii ya kunde ilizalishwa mwaka 1992 na Kituoa cha Utafiti cha Ilonga kwa ushirikiano na Naliendele.
 
2.FAHARI
Aina hii hukomaa kwa siku kati ya 75 – 90. Mmea husambaa na maua yana rangi ya zambarau. Mbegu zake ni za mviringo. Hustawi maeneo yenye mwinuko wa mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Hutoa hadi tani 3 kwa hekta moja (kilogram 600 - 1500 kwa ekari ). Huvumilia magonjwa ya CABMV na mabaka. Fahari ilitolewa mwaka 1982 na Kituo cha Utafiti Ilonga kwa kushirikiana na Naliendele
 
3.VULI_1
Inakomaa kwa siku 55 – 65. Hukua ka kunyooka na kusambaa kidogo. Mbegu zake ni nyekundu na za mviringo. Inastawi vizuri maeneo yenye mwinuko wa mita 0 – 1500 toka usawa wa bahari. Ikipataiwa matunzo mazuri huto hadi tani 2 kwa hekta moja (Kilogram 450-800 kwa ekari). Vuli – 1 inavumilia CABMV, BP na BB Vuli – 1 ilizalishwa mwaka 1987 kutoka kituo cha utafiti Ilonga.
 
4.VULI_2
Inakomaa baada ya siku 65 – 70 baada ya kupandwa inaota ikiwa imenyooka na kusambaa kidogo. Mbegu zake zina weupe uliofifia na ni mviringo. Aina hii husitawi vizuri maeneo yenye mwinuko wa mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Katika matunzo mazuri aina hii huzalisha hadi tani 3.5 kwa hekta moja(Kilogram 800 -1200 kwa ekari) . Vuli – 2 huvumilia CABMV, BP na BB Vuli – 2 ilizalishwa mwaka 1987 kutoka kituo cha utafiti Ilonga.
 
KUPANDA KUNDE
Kunde hupandwa mwishoni mwa msimu wa mvua ili kuziepusha kukauka wakati mvua inaendelea kunyesha.na pia unweza kupanda wakati zao jingine linakaribia kuvunwa au katika shamba lilivunwampunga na lina unyevu wa kutosha.Muda mzuri wa kupanda kunde ni akuanzia mwezi Februari mwishoni hadi Machi na Aprili kwa maeneo ambayo mvua huchelewa kuisha.
 
kuisha.KUMBUKA mbegu zinazotambaa za kunde zipandwe miezi miwili kabla ya mvua kuisha kwani hizi huchukua siku nyingi kukomaa na Mbegu zinazosimama zipandwe mwezi mmoja kabla ya mvua kuisha.
Kunde huitaji kiasi cha kilogram 4-12 za mbegu kwa ekari.kiasi cha mbegu kitategemea ukubwa wa mbegu,(mbegu kubwa zitahitajika kilogram nyingi) nafasi za upandaji,Ukipanda karibu karibu na mbegu itahitajika nyingi,Ubora wa mbegu katika uhotaji.Zisizoota vizuri huitaji mbegu nyingi zaidi
 
NAFASI YA UPANDAJI
Unaweza kutumia nafasi zifuatazo kwa kupanda kunde zako
KUNDE ZINASOSIMAMA-Tumia sentimeta 45 hadi 50 mstari hadi msatari na sentimeta 15 hadi 20 shina hadi shina katika mstari / Sm ( 50 X 20 )
KUNDE ZINAZOSAMBAA-Tumia nafasi ya Sentimeta 70 hadi 75 mstari hadi mstari Kwa sentimeta 25 hadi 30 shina hadi shina katika mstari / Sm ( 75 X 30 )
Panda kwa kufikia kiasi cha sentimeta 2.5 hadi 5 ardhini na tumia mbegu tatu kwa kila shimo na baadaye punguza uache 2 kwa kila shimo kama unauhakika wa mbegu zako unaweza kupanda moja kwa moja mbili mbili kwa shimo
 
MBOLEA

SAMADI NA MBOLEA ZA VIWANDANI
Kama shamba lako halina rutuba ya kutosha unaweza kuongeza samadi kiasi cha tani tano kwa ekari moja na uhakikishe mbolea hii imemwagiwa au imenyeshewa na mvua ya kutosha kuiozesha kabla ya kupanda kunde zako na pia unaweza kupanda kwa kutumia mbolea ya TSP kiasi cha Kg 50 kwa ekari na baadaye kuzia mbolea ya SA kiasin cha Kg 50 kwa ekari.
 
Back
Top Bottom