Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuna baadhi ya wakulima mazao yao yamenyauka na kufa yakiwa ndani ya green house, kuna wakulima walijenga green house kwa matumaini ya kupata pesa ya haraka na wameishia kupata hasara kwa kuwa hawakupata ushauri sahihi na mazao yao yamekauka pia kama vile yapo kwenye shamba la wazi.
 
Mara nyingi green house hizi zimekuwa kwenye eneo lenye joto kubwa ikilinganishwa kuwa kimo chake kinapaswa kuwa chini ya mita 2.5, hivyo kufanya joto kuwa kali sana na mazao kunyauka, ambapo wataalamu wanashauri kuwa ni bora zaidi kujengwa kulingana na mazingira ya eneo au mkoa husika
 
Mavuno kidogo.

Wapo wakulima waliolima ndani ya green house, mbali ya kwamba walikuwa wakiaminishwa kuwa watapata mavuno mengi yatakayowafanya kurudisha gharama zao ndani ya msimu mmoja matokeo yake imekuwa kinyume kabisa (mavuno hafifu na yasiyo bora) jambo ambalo linatokana na kutozingatia kanuni bora za uandaaji wa aina hii ya kilimo.
 
Kukosekana kwa soko

Baadhi ya wakulima waliowekeza kwenye kilimo hiki wamekuwa wakiaminishwa kuwa kwa kuwa ni mavuno ya green house, basi yatapata soko zuri muda wowote atakaovuna, jambo ambalo ni kinyume ambapo kwa sababu hizo wamekuwa wakizalisha mazao bila ya kuwa na hofu ya kukosa soko.
 
Wataalamu wa kilimo hiki wanasema kuwa kwanza kabisa ili mtu aweze kufanikiwa basi hana budi kuhakikisha kuwa anaweka juhudi, umakini na malengo katika jambo husika, kwani unaweza kuwa na green house lakini bado ukaambulia hasara na usifaidike na chochote kinyume na matarajio yako.
 
Hii itakusaidia kujua changamoto na namna gani unavyoweza kuzikabili ikiwamo, gharama, magonjwa kwani usipokuwa makini unaweza kujikuta unakabiliana na changamoto zilizoko kwenye kilimo cha kawaida cha shamba wazi ilihali una green house.
 
Back
Top Bottom