Nafikiria kwamba ametazama hili kwenye michezo ya video ya kompyuta au kwenye runinga. Sijui iwapo alifahamu hasa nini alichokuwa anakifanya. Siwezi kujibu hilo. Najua tu kwamba ni mkasa, kisa cha kusikitisha."
Mama ya watoto hao alikuwa kwenye chumba kingine, akiwalicha watoto wengine kisa hicho kilipotokea.
Polisi wanachunguza kisa hicho, ikiwa ni pamoja na jinsi mtoto huyo aliweza kuifikia bastola hiyo ya risasi za kiwango cha .25.
"Hili ni jambo geni sana kwetu, hatujawahi kukumbana na mtoto wa miaka tisa aliyempiga risasi mtoto mwenzake," liwali Cantrell aliambia vyombo vya habari