Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu kifungo cha miaka saba jela raia wa Kenya, Stanley Murithi baada ya kumtia hatiani kwa makosa 419 yakiwamo ya utakatishaji wa fedha.
Akitoa hukumu hiyo leo Jumanne Machi 20, 2018, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 15 wa upande wa mashtaka pamoja na utetezi wake mshtakiwa mwenyewe, atatumikia adhabu hiyo.