Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

UKWAJU MTI WENYE MATUMIZI LUKUKI : Asili ya mti huu ni ukanda wa nchi za tropiki, unaojumuisha nchi za Sudan na Madagaska. Baadaye ulipelekwa India huko ndipo ulipoanza kupata umaarufu na kuonekana kama ndiyo asili yake. Mti huu ulianza kuenea sehemu mbalimbali duniani kama vile nchi za Ghuba ya Uajemi na Uarabuni ambapo huko uliitwa ‘tamar hind’(tamarind) wakimaanisha kwamba ni mtende wa India.
 
Kuanzia wakati huo mti huu ulianza kupata umaarufu sehemu mbalimbali duniani kote kutokana na kuwa hazina kubwa kilishe, ki-tiba na hata kimapambo, baadhi ya matumizi yake ni kama yafuatayo:
 
Tunda la mti huu hutumika kama kiungo muhimu katika utayarishaji wa vyakula mbalimbali ili kuviongezea ladha vyakula hivi. Pia lina virutubishi vingi vinavyohitajika mwilini kama sukari, aina ya tindikali zenye vitamini kama citric acid, malic acid na vinginevyo vingi, kwa mfano, hutumika kama chachandu katika chips na nyama.
 
Tunda la ukwaju linapokorogwa na maji na sukari na kuhifadhiwa kwenye ubaridi hutoa kinywaji kitamu na kinachopendwa na watu wengi duniani
 
Vilevile katika baadhi ya nchi za Mashariki ya mbali kama Thailand hutumia mbegu za tunda la mkwaju kutayarisha kahawa mbadala.
 
MATUMIZI KATIKA TIBA

Utomvu unaotokana na majani ya mkwaju yaliyokaushwa na kuchemshwa na kupakwa husaidia kuondosha uvimbe kwenye macho (conjuctivitis), kuponya kuharisha damu (Dysentry) na manjano mwilini (Jaundice), mgoro na magonjwa mbalimbali mengine.
 
Magome ya mti huu yanaposagwa na kupakwa mwilini husaidia kuondoa mafuta ya ziada kwenye ngozi na kuharakisha damu kuganda na hivyo kuzuia upotevu wa damu nyingi mwilini wakati wa ajali.
 
Vilevile juisi ya ukwaju huweza kuwasaidia watu waliopooza viungo vya mwili kuweza kupata nafuu au wakati mwingine kuweza kuondokana kabisa na tatizo hilo, pia huweza kuondosha nguvu za ulevi mwilini na maumivu ya kichwa yanayosababishwa na kupigwa kwa muda mrefu na jua la usoni
 
Majimaji yakamuliwayo kutoka kwenye mmea wa mkwaju yanapochanganywa na vitu vingine kama asali, ndimu na tende huweza kuondosha maumivu na uvimbe unaosababishwa na wadudu pia matatizo ya kuvimbiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…