Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Zao hili hupendelea kipindi kirefu cha jua na mvua za wastani. Hali ya mvua nyingi pamoja na baridi kali husababisha mashambulizi ya magonjwa na wadudu. Vilevile joto jingi, mwanga kidogo pamoja na hali ya unyevunyevu husababisha magonjwa mengi kuenea na mmea kuwa na majani mengi.
 
HALI YA UDONGO

Udongo wa kustawisha nyanya yabidi uwe na rutuba ya kutosha.

• Unaweza kutumika samadi au mbolea ya takataka iliyooza vya kutosha. Mbolea ichanganywe vizuri na udongo mapema kabla ya kupanda. Kiasi cha mbolea cha kuwekwa bustanini hutegemea kupatikana kwake pamoja na hali ya udongo. Mathalani wastani wa tani 5 hadi 6 zatosha kwa robo hekta ya bustani.
 
Iwapo ni vigumu kupata samadi, mkulima anashauriwa kutumika mbolea ya chumvichumvi. Kwa wastani mahitaji ya robo hekta ya bustani ni kama ifuatayo: Wakati wa kupanda weka kilo 50 za Triple Super Phosphate na wakati ikikua weka kilo 50 za Sulphate of Ammonia au Calcium Ammonium Nitrate. Ni muhimu kuhakikisha mbolea inawekwa mbali na shina ili kuepuka uwezekano wa kuunguza mashina. Pia hakikisaha ardhi ina unyevu wa kutosha wakati wote.
 
KUPANDA:

• Mbegu za nyanya hupandwa kwenye kitalu ambapo hukaa mpaka miche itoe majani makubwa mawili, yaani baada ya wiki 6 hadi 8 kisha huhamishiwa bustanini. Baadhi ya wakulima hutawanya moja kwa moja shambani. Hata hivyo inabidi hupunguza kazi ya kupandikiza lakini yabidi kupunguza miche baada ya kuota.
 
Umbali kati ya mimea hutegemea rutuba ya ardhi na aina ya nyanya. Kwa wastani hatua zinazopendekezwa kupandikiza ni sentimita 30 toka mche hadi mche na sentimita 90 kati ya safu na safu. Kwa kutumika hatua hizi, robo hekta ya bustani huwa na mimea 7,500. Upaliliaji wa bustani hufanywe mara kwa mara. Si busara kutifua kwa chini sana (zaidi ya sentimita tano) kwani kufanya hivyo kuna hatari ya kukata mizizi ya mmea.
 
Kupunguza matawi: Baadhi ya wakulima wana desturi ya kupunguza matawi na kufungia kwenye viguzo yanayobaki. Matawi yote ambayo hujitokeza kati ya mashina makubwa hukobolewa yakiwa bado madogo. Kazi hii hurudiwa kila baada ya majuma mawili. Wakati wa kufungia mimea kwenye viguzo uangalifu ufanywe ili kamba zisibane mashina na kuzuia ukuaji mzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…