MBOLEA INA FAIDA KUBWA KWA WAKULIMA : Utumiaji wa mbolea katika karne hii ni jambo lisiloepukika. Hii ni kutokana na ukweli kwamba ardhi zetu nyingi zimechoka baada ya kilimo cha muda mrefu na kuongezeka kwa idadi ya watu.
Takwimu za ongezeko la idadi ya watu duniani zilizotolewa na Benki ya Dunia inaonyesha kwamba idadi ya watu duniani Itaongezeka kutoka watu bilioni 6 mwaka 1999 mpaka bilioni 7 ifikapo mwaka 2020. Takribani mpaka asilimia 90 ya chakula cha kukidhi mahitaji maongezeko haya lazima kipatikane kutoka mashamba ambayo tayari yanalimwa.
Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) lilikadiria kwamba kipindi cha mwaka 1995 mpaka 1997 kiasi cha watu milioni 790 katika nchi zinazoendelea hawakuwa na chakula cha kutosha. Hata hivyo katika miaka ya karibuni idadi hiyo imekuwa ikishuka kwa wastani wa watu milioni 8 kwa mwaka.
Lakini hali hii isipobadilika ifikapo mwaka 2015 wastani wa watu milioni 600 watakumbwa na njaa. Idadi kubwa ya chakula katika nchi zinazoendelea huzalishwa na wakulima wadogo wadogo ambao ni masikini waishio vijijini. Hivyo Uanzishaji wa mifumo bora ya kilimo na uboreshaji wa mbinu zake siyo tu kutatuhakikishia mapato zaidi, bali pia chakula cha kutosha kukidhi ongezeko la watu.
Samadi ndiyo msingi wa kufanikisha mbolea za viwandani
Kabla ya kutumika mbolea za viwandani ni vyema kwanza utumie mbolea ambazo asili yake ni viumbe hai, kwa mfano vinyesi vya kuku, ng,ombe mabaki ya mbogamboga na aina ya nafaka. Hivi vyote lazima vichanganywe na kuozeshwa vyema kabla ya kutumiwa shambani.
Hata hivyo, itabidi ikumbukwe kwamba mbolea hizi hazina virutubishi vya kutosha na viwango vyake hubadilikabadilika, na mara nyingi hazipatikani kwa kiwango kinachohitajika. Hivyo mbolea za viwandani lazima kutumiwa sambamba na mbolea-ozo.