Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Aina nyingine ya wadudu wanaokufa muda mfupi tu baada ya kula majani au sehemu nyinginezo za mmea zilizonyunyiziwa dawa ya muarobaini ni kama vile viwavijeshi ambao hufa siku 2 au 3 baada ya kula mimea iliyonyunyiziwa dawa ya muarobaini.
 
Kuna wadudu wengine ambao huathirika kwa kubadili mwenendo au tabia zao na kupoteza uwezo wa kutaga mayai. Isipokuwa kuna aina za wadudu ambao wanaathirika kidogo sana, au hawapati madhara yeyote kutokana na madawa ya muarobaini.
 
JINSI YA KUTAYARISHA DAWA YA MUAROBAINI
• Kwa kawaida matunda ya muarobaini hudondoshwa chini na wadudu kama ndege, popo na wengineo hivyo basi mbegu zilizokwishamenywa zinaweza kuokotwa chini ya mti huu. Iwapo mbegu nyingi zinahitajika basi unaweza kuutingisha mti na kuokota matunda yanayodondoka.
 
Loweka matunda kwenye maji na sugua kwa viganja viwili au juu ya chekeche kubwa. Kwa kuwa kuvuna mbegu kwa kutingisha ni kazi kubwa kuliko kuokota zilizodondoshwa na ndege.
 
Baada ya kuzitoa maganda mbegu hazina budi kusafishwa kikamilifu. Utoaji wa maganda husababisha ukuaji mzuri wa mbegu. Mbegu zisipooshwa na zisipokaushwa vizuri zitaota ukungu ambao hupunguza nguvu ya dawa hii ya kuulia wadudu, ili kuepuka kuota ukungu mbegu hazina budi zikaushwe vyema vema bila kulaliana, na zianikwe kwenye kivuli sehemu ya uwazi kwa siku kadhaa hadi zikauke
 
Ili kuepusha ukungu kwenye mbegu baada ya kukauka mbegu zinapasa kuhifadhiwa kwenye vyombo vyenye hewa ya kutosha kama vile magunia matupu.
 
Unga wa mbegu za muarobaini unachanganywa na maji na kukorogwa vizuri. Mchanganyiko huu uwachwe kwa muda wa saa 5-6 au usiku mzima ili uwe mkali zaidi. Robo kipande cha sabuni kilainishwe na kiongezwe kwenye mchanganyiko huu kabla ya kunyunyizia. Hii inasaidia dawa ishike vizuri kwenye majani. Ni muhimu kuhakikisha unakoroga vyema wakati unapoweka unga wa mbegu za muarobaini ndani ya maji.
 
Changanya kilo moja ya muarobaini kwa debe moja la maji au gramu 50 za mbegu zinahitajika kuchanganywa na lita 1 ya moja. Kama hakuna mizani inawezekana kutumia vifaa vya kupimia ujazo kama makopo, madebe ili mradi ujazo unaohusika ujulikane.
 
Endapo hakuna mbegu majani ya muarobaini yanaweza pia kutumika, toa majani kutoka kwenye matawi. Kiasi cha gramu 40 za majani zinahitajika kuchanganya na lita 1 ya maji. Kiasi hiki kinalingana kwa kukadiria na kiganja kimoja kilichojaa cha majani. Changanya kiasi sahihi cha maji na uache mchanganyiko huu kwa muda wa masaa 12.
 
Kabla ya kunyunyiza dawa hii kwenye mmea, chuja mchanganyiko huu ongeza na sabuni kiasi. Matumizi ya mchanganyiko huu wa majani ni sawa kabisa na ule wa mbegu za muarobaini.
 
Back
Top Bottom