Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Saratani : Alovera ina viambato vingi ambavyo husaidia kuzuia kansa. Mathalani, kansa ya mapafu huweza kudhibitiwa kwa kutumia bidhaa zenye alovera. Zaidi ya hapo tafiti nyingi zimethibitisha kwamba utomvu wa mmea huu huzuia kuzaliana kwa chembechembe za kansa.
 
Maumivu ya misuli na viungo : Utomvu wa alovera huzuia maumivu ya misuli na viungio vya mwili. Mathalani tindikali ipatikanayo kwenye alovera imethibitika kuponya kwa kiasi kikubwa maumivu ya misuli kwa asilimia 79 na kiambatanishi kingine kijulikanacho kama Anthraquinone huzuia maumivu kwa asilimia 67.3. Aidha imethibitika kutoathiri shughuli za utendaji wa kinga za mwili.
 
Ukimwi : Sukari ijulikanayo kama mannose iliyopo kwenye utomvu wa mmea huu huzuia mashambulizi ya kirusi cha HIV-1 ambacho husababisha ukimwi. Mathalani muathirika wa ugonjwa huu atapewa vikombe 9 vya juisi ya mmea huu kwa siku 90, na humuongezea nishati kinga za mwili.
 
Vidonda vitokanavyo na maradhi ya ngozi : Utafiti mmoja uliofanyika kwa wagonjwa 60 waliokuwa wakisumbuliwa na maradhi haya walitibiwa kwa mgando wa utomvu wa alovera. Walikuwa wakipakwa mara 3 kwa siku 5 na waliweza kupona kabisa baada ya miezi 8.
 
Kuondosha sumu mwilini : Kutokana na kukosa mipangilio ya lishe asili, binadamu amekuwa na changamoto ya kukabiliana na rangi zitumikazo kwenye vyakula, viambato vya ladha na hifadhi ya vyakula mbalimbali. Viambato hivi hupenya haraka kwenye damu na hapo hukusanyika na kuhifadhika kama sumu hatari. Hata hivyo unywaji wa kikombe kimoja cha juisi ya alovera hutosha kuondosha sumu hii mwilini.
 
Uzalishaji wa damu : Tafiti zimeonyesha kwamba ni vigumu kwa mtu kuwa na ujazo sahihi wa damu mwilini na pia mtu hawezi kuwa na hali nzuri kiafya kama damu yake ipo chini ya kiwango kinachokubalika. Alovera huhamasisha viungo vya mwili kuongeza uzalishaji wa damu mwilini. Pia ina viinilishe muhimu vihitajikavyo kwa uzalishaji wa damu.
 
Kukosa nguvu za kiume : Kwa muda mrefu alovera imekuwa ikitumiwa kama dawa ya kuongeza nguvu za kiume. Utomvu wake huongeza kiasi cha manii kwa wanaume ambayo huchochea hamu ya tendo la ndoa. Hata wanawake ambao mifumo yao ya uzazi imeziba hurejea katika hali ya kawaida baada ya miezi 6 ya matibabu kwa kutumia mmea huu.
 
Kuangamiza minyoo mwilini : tafiti zimeonyesha kwamba watu wengi hawana mazoea ya kuangamiza minyoo katika miili yao mara kwa mara, mamia ya minyoo huzaliana wakati wote. Ni muhimu kuaangamiza minyoo kila baada ya miezi 3 hadi 4. Pia ni hatari kutegemea njia rahisi za kuangamiza minyoo kwa vile nyingi ni bandia na hazitibu. Hivyo tiba hii ya mitishamba ndiyo njia pekee ya kuangamiza minyoo. Utomvu wa mmea huuhusafisha tumbo. Ukichanganywa na mitishamba mingine huimarisha sehemu hizi.
 
Kuvimbiwa : Moja kati ya mambo ya kudhalilisha ni urefu wa muda ambao mtu hukaa chooni mpaka amalizapo haja yake. Kwa kawaida mtu huenda mara 3 kwa siku, wengine mara mbili au chini ya hapo. Vilevile watu huchukua muda mrefu kwenda haja licha ya ukweli kwamba wanapata milo yao kawaida na wengine vyakula walavyo havisagwi kikamilifu mwilini. Vyakula hivi vikwamavyo mwilini hukusanyika kwenye utumbo mpana na kusababisha vitambi. Watu wengi huchukulia hali hii kama kusitawi kimaisha. Hivyo utumiaji wa shubiri husaidia huondoa matatizo ya usagaji chakula na kwenda haja.
 
Kukosa usingizi : Hali hii husababishwa na hali mbalimbali ambazo hutofautiana baina ya mwathirika mmoja na
mwingine. Mlundikano wa mawazo ukiambatana na ukosefu wa tiba ndiyo hupelekea hali hii. Alovera hufanya kazi hufufua utendaji mzuri wa kazi fulani mwilini na huwezesha mwili kurejea hali yake ya kawaida pia na huchochea mtu kupata usingizi.
 
Vilevile ulafi kupita kiasi nyakati za usiku hupelekea ukosefu wa usingizi, Mtu hufumba macho tu wakati sehemu zingine za mwili zikiendelea kufanya kazi ya kusaga wa chakula na kukisambaza sehemu mbalimbali mwilini. Hali hii huchochea ya kukosa usingizi. Lakini utumiaji wa alovera huharakisha usagaji na ugawaji chakula mwilini, hivyo kufanikisha upataji usingizi.
 
Pumu : Alovera hufahamika vizuri kwa uwezo wake wa kuyapa uhai mapafu, husaidia utendaji wake wa kazi na hudhibiti shughuli mbalimbali za mfumo mzima wa upumuaji. Mmea huu unapochanganywa na mitishamba mingine hutoa nafuu kwa wagonjwa hao.
 
Maumivu ya kichwa : Hii husababishwa na kukithiri kwa kazi, utumiaji uliokithiri wa madawa au matumizi yasiyokusudiwa ya madawa haya. Utumiaji wa alovera husafisha mifumo mbalimbali ya mwili na hivyo huondosha hali hii.
 
Maumivu ya mgongo : Takribani kila mtu kwa wakati fulani husumbuliwa na maumivu ya mgongo, kuna sababu mbalimbali za hali hii. hata mazingira tunamoishi huchangia, Hata hivyo tafiti zimethibitisha kwamba watu huathiriwa na namna ya maisha wanayoishi. Hivyo kutumia mmea wa alovera hudhibiti hali hii.
 
Maradhi ya fungasi : aina zote za mashambulizi ya fangasi hudhibitiwa kwa kutumia aloevera. Baadhi ya watu hawawezi kuvaa viatu muda mrefu kwa sababu huathiriwa na fangasi. Hivyo inashauriwa waoshe miguu yao mara kwa mara kwa maji yaliyochanganywa na unga wa aloevera. Vilevile inapendekezwa kuoga kwa maji ya moto yaliyochanganywa na wa alovera ili kuwa na ya ngozi yenye afya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…