Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Endapo zao la soya litaonekana kushambuliwa na wadudu shambani, mkulima anashauriwa kutumia dawa za wadudu kama vile Thiodan 35% EC na Sumithian 50% EC kwenye kipimo cha milimita 40 za dawa na lita 20 za maji. Au kipimo kilichopendekezwa kwa dawa husika. Upulizaji wa dawa ufanywe kulingana na kiwango cha shambulizi la wadudu.
 
Magonjwa ya soya ni machache. Wakati mwingine zao linaweza kushambuliwa na vinyemelea vya ukungu na bakteria. Magonjwa haya huenezwa kupitia mbegu au masalia ya mimea shambani na wadudu aina ya mafuta. Ili kuepuka magonjwa haya, mkulima anatakiwa kuzingatia mbinu za kilimo bora na ushauri wa kitaalam, kama kupanda mbegu safi sehemu husika au kupanda kwa mzunguko unaojumuisha mazao yasiyoshambuliwa na magonjwa ya soya, kama alizeti na mahindi.
 
Soya hukomaa katika kipindi cha miezi 3 hadi 7. Kipindi hicho hutegemea aina, mahali inapopandwa na utunzaji wa shamba. Mfano aina ya Bossier hukomaa kwa miezi 3 hadi 4, wakati Uyole Soya 1 miezi 4 hadi 5. Inashauriwa kuwahi kuvuna mara ikomaapo na kukauka ili kuzuia upotevu wa zao shambani. Pia wakati ambao jua siyo kali, kama asubuhi ili kuepuka kupasuka kwa mbegu na kupuputika chini.
 
Uvunaji hufuatiwa na kupura. Soya haitakiwi kupigwa kwa nguvu kwa sababu mbegu yake hupasuka kirahisi. Baada ya kupura, takataka na uchafu mwingine huondolewa kwa kupepetwa na kupembuliwa. Kisha hukaushwa mpaka kubakia asilimia 10 ya unyevu ndani ya mbegu, hapo huwa tayari kuhifadhiwa ghalani kwa matumizi au kusubiri soko. Kwa kawaida, mavuno ni kilo 1500 hadi 2500 kwa hekta. Ukubwa wa mavuno hutegemea aina, hali ya hewa, rutuba ya udongo, matumizi ya mbolea, na utunzaji wa jumla wa shamba.
 
BfwyigJgZwO.jpg
 
Back
Top Bottom