Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

BgoedUPAp74.jpg
 
Hata hivyo Bassier ndiyo aina ambayo hustawi katika maeneo mengi nchini. Kwa wastani aina mbalimbali za soya huchukuwa wastani wa miezi mitatu hadi saba kukomaa. Muda huo hutegemea aina ya mbegu, mahali ilikopandwa, na kiwango cha matunzo shambani.
 
Utayarishaji ni pamoja na kuondoa magugu shambani. Zao hili halivumilii magugu, hususani katika hatua za mwanzo za ukuaji. Shamba la soya laweza kulimwa kwa sesa au matuta. Kilimo cha matuta kinashauriwa sana katika maeneo ya miinuko, pia sehemu zilizo tambarare zenye mvua nyingi. Sababu ni kuepuka madhara ya maji yanayotuama baada ya mvua kubwa kunyesha.
 
Upandaji unaoshauriwa ni sentimita 10 kwa 45 kwa soya fupi kama Bossier, na kwa soya ndefu kama Uyole Soya 1 nafasi kati ya mmea na mstari iwe sentimita 10 kwa 60. Kwa kawaida mbegu moja hupandwa kila shimo na hufunikwa kwa kina cha sentimita 2 hadi 5. Sababu ya kufunika ni kuepusha kuharibiwa au kuliwa na wanyama kama panya. Pia ni vyema kuhakikisha kwamba mbegu inapandwa kwenye udongo wenye unyevunyevu. Haishauriwi kupanda katika udongo mkavu au kuloweka mbegu.
 
Palizi hufanywa wiki mbili baada ya mbegu kuota. Palizi ya pili itategemea na kiwango cha magugu shambani. Kama magugu yatakuwa yamefunikwa na majani ya soya basi siyo lazima kupalilia mara ya pili. . Magugu yanaweza kudhibitiwa kwa kutumia dawa ya GALEX.
 
Back
Top Bottom