Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

That ass[emoji7] [emoji7] [emoji7] [emoji7] [emoji7]
Like yours babe [emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️
 
IMG_3300.JPG
 
Nilikuwa sijui kuwa Magimbi yanafaida sana mwilini! Hivi vyakula vyetu vya [HASHTAG]#Uswahili[/HASHTAG] japo wengine wana vidharau lakini ndio tiba kwa magonjwa yote yanayo toka na na kula vyakula vya “kizungu” haya ona faida za kula magimbi nipamoja na
Pia kula magimbi kwa sana kwapelekea uwezekano mkubwa wa kupata mimba ya mapacha.
 
Zlatan Ibrahimovic amekamilisha uhamisho wake wa kwenda LA Galaxy akionyesha picha yake pamoja na Simba.

Ibrahimovic anayejifananisha na Simba alituma video yake akiwa na jezi ya Galaxy: "Los Angeles, karibu Zlatan."

Ibrahimovic na Manchester United wameamua kuchana mkataba uliokuwepo baina yao na staa huyo wa kimataifa wa Sweden jana alitazamiwa kuendelea na maisha mengine kwa kujiunga na klabu ya LA Galaxy.

Dili la Zlatan kwenda Galaxy linatazamiwa kuwa mkataba wa pauni 1 milioni kwa mwaka na lilitazamiwa kutangazwa kama tangazo katika ukurasa mzima wa gazeti maarufu la Marekani, Los Angeles Times na alitazamiwa kwenda California kwa ajili ya kutambulishwa.
 
  • Thanks
Reactions: Soe
Zlatan mwenye umri wa miaka 36 amesaini mkataba mpaka mwishoni mwa msimu na anaweza kucheza mechi yake ya kwanza kwa wababe hao katika pambano la Ligi Kuu ya Marekani dhidi ya watani wao wa jadi LAFC Machi 31.

United ilithibitisha jana kwamba walikuwa wameukomesha mkataba wa staa huyo ambaye kwa mara ya kwanza sasa atacheza nje ya bara la Ulaya baada ya kutamba katika klabu za Barcelona, Ajax, Paris Saint-Germain, Juventus, Inter Milan na AC Milan.

Zlatan mwenyewe aliandika katika mtandao wake akisema “Mambo mazuri ufika mwisho na huu ni wakati wa kuendelea na maisha mengine baada ya kuwa na misimu mizuri miwili na Manchester United.”

“Asante sana kwa klabu, mashabiki, timu, kocha na wafanyakazi wengine ambao walishirkiana na mimi katika sehemu hii ya historia yangu.:”

Zlatan alikuwa akihusishwa kwa muda mrefu kujiunga na klabu hiyo ambayo iliwahi kuwachukua David Beckham na Steven Gerrard katika nyakati mbalimbali na sasa Zlatan anakwenda kufungua ukurasa mpya klabuni hapo.
 
  • Thanks
Reactions: Soe
Malkia wa Muziki wa injili nchini, Rose Muhando atazindua albamu yake mpya ya ‘Usivunjike Moyo’ katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Mkurugenzi wa Msama Promotins, Alex Msama amesema waimbaji wote watakaoshiriki tukio hilo linalosubiriwa kwa hamu, kwa sasa wapo katika mazoezi.

Alisema ya kwamba, awali tamasha hilo lilikuwa lifanyike katika mikoa miwili tu ya Mwanza hapo (Aprili Mosi) na Simiyu (Aprili 2), lakini sasa litafanyika pia mkoani Dodoma katika Uwanja wa Jamhuri Aprili 8.
 
Tumeamua kuongeza kituo kingine cha tatu kwa ajili ya tamasha la Pasaka la mwaka huu, hivyo baada ya Mwanza na Simiyu, Aprili 8, uhondo utakuwa Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma,” alisema.

Waimbaji wengine katika tukio hilo ni Angel Benard, Paul Clement, Christina Shusho, Beatrice Mwaipaja, Bonny Mwaitege, Ephraem Sekereti kutoka Zambia, Jesca Honole na wakali wengine.

Viingilio vya tukio hilo ni kwamba, katika Uwanja wa CCM Kirumba; wakubwa watalipa Sh5,000 huku watoto wakilipa Sh2,000 na mkoani Simiyu; wakubwa watalipa Sh3,000 na watoto itakuwa Sh2,000.

Msama alisema mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba katika tamasha la Mwanza litakalofanyika Uwanja wa CCM Kirumba.

“Mara zote baadhi ya waimbaji wamekuwa wakiimba live kwa kutumia vyombo jukwaani, hata safari hii itakuwa hivyo ili kuongeza mvuto zaidi kwa kila atakayefika uwanjani,” alisema Msama.
 
JACK Wilshere amefichua kuwa ameambiwa na Kocha Arsene Wenger aondoke Arsenal.
Wilshere aliripotiwa kuwa kwenye mazungumzo ya mkataba mpya wa kuendelea kubaki Emirates, lakini amedai Kocha Wenger amemshauri tu akatafute timu nyingine ya kuichezea.
“Aliniambia ‘nataka kuwa mkweli kwako kwa wakati huu hatuwezi kukupatia mkataba mpya. Hivyo, kama watakupigia simu huko kwingineno, unaweza kwenda,’" alisema Wilshere akifichua kile alichoelezwa na Wenger
 
Nilikuwa gym kwa wakati huo, nikaduwaa sikutoka chumbani. Kilikuwa kitu cha kushangaza kidogo, labda kuna waliokuwa wakilifahamu hilo, nilichokuwa nakitaka ni kupata uhakika tu kuwa klabu inanichukuliaje.
“Nilisema napigania namba yangu. Na siku zote nilikuwa na uhakika nitarudi na kupata namba kwenye kiungo pindi nitapokuwa fiti bila ya kusumbuliwa na majeraha. Nilithibitisha hilo na nilirejea kwenye timu."
 
Wilshere alisema hilo lilitokea kwenye dirisha lililopita ambapo Kocha Wenger aliamua tu kuwa mkweli kwa kumwaambia vitu bayana.
Kiwango cha Wilshere kwa siku za karibuni kimerejea kwenye ubora wake na kufanikiwa kupata namba katika Timu ya Taifa ya England, ambayo ipo kwenye maandalizi kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika baadaye mwaka huu huko Russia.
 
KUNA baadhi ya mastaa ambao hauwezi kuamini kwamba waliwahi kucheza timu moja katika siku za nyuma. Kila ukijaribu kuunganisha matukio unapata wakati mgumu kuamini kuwa waliwahi kucheza timu moja wakati fulani
 
  • Thanks
Reactions: Soe
Dele Alli na Alan Smith - MK Dons

Mpaka sasa Alli ana umri wa miaka 21 tu na anatamba katika Ligi Kuu ya England. hauwezi kuamini kwamba kila unapowaza kuhusu maisha ya staa wa zamani wa Leeds United na Manchester United, Alan Smith unakosa kujua ni namna gani mkongwe huyu mwenye umri wa miaka 37 sasa alicheza na Alli mahala. Ni kweli, walikutana katika klabu ya MK Dons ya daraja la kwanza. Wakati Alli alianza kuchanua na maisha yake ya soka, Smith alikuwa anaelekea mwisho katika maisha ya soka.
 
  • Thanks
Reactions: Soe
Aguero na David De Gea - Atletico Madrid

Timu mbili za Manchester ziliyaachanisha maisha yao ya soka. Kila mmoja kwa sasa ni mchezaji muhimu na anayeheshimika sana katika timu yake lakini usishangae kuona Aguero na De Gea wakipiga stori mara baada ya kumalizika kwa pambano la watani wa jadi wa jiji la Manchester. Wawili hawa waliwahi kukipiga pamoja katika klabu ya Atletico Madrid kabla ya Aguero kwenda Man City na De Gea kwenda Man United.
 
Marouane Chamakh na Mauricio Pochettino - Bordeaux

Unaweza usiamini hili kwa sababu kwa sasa mmoja ni mshambuliaji ambaye anamaliza siku zake za kucheza soka la juu, wakati mwingine ni kocha mkali anayekuja juu katika klabu ya Tottenham Hotspurs. Wanaonekana kuwa watu wawili tofautu lakini ukweli ni kwamba wawili hawa waliwahi kucheza pamoja katika klabu ya Bordeaux ya Ufaransa. Baadaye Pochettino alikwenda klabu ya Espanyol alikomalizia maisha soka, wakati Chamakh alikwenda Arsenal kwa uhamisho huru.
 
Ramsey na Hasselbaink - Cardiff City

Kwa haraka haraka akili yako inakutuma kwamba Hasselbaink alicheza wapi? Ni wazi kwamba utawaza zaidi Leeds United na Chelsea. Ramsey? Yupo Arsenal. Hata hivyo wawili hawa waliwahi kukutana katika klabu ya zamani ya Ramsey Cardiff City. Wakati Hasseibaink alikwenda huko kumalizia maisha yake ya soka, Ramsey alikuwa anaanza kuwika kiasi cha kuwindwa na klabu kubwa kabla ya kutua Arsenal. Walicheza pamoja mwaka 2007.
 
  • Thanks
Reactions: Soe
Dimitri Payet and Joe Cole - Lille

Wote wamewahi kucheza West Ham kwa nyakati tofauti. Lakini hii haimaanishi kwamba wawili hawa hawajawahi kucheza katika timu moja. Ukweli ni kwamba wote walikutana katika klabu ya Lille ya Ufaransa wakati Cole alipoamua kufunga safari yake ya nje ya nchi tofauti na wachezaji wengi wa Kiingereza. Dunia ni ndogo.
 
Back
Top Bottom