Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MUDA WA KUPANDA

Viazi mviringo mara nyingi katika maeneo mengi vinapandwa agost hadi september na november hadi December. Natumia sentimita 60 hadi 75 kutoka mstari hadi mstari na nafasi kati ya kiazi na kiazi ni sentimita 30.
 
MBOLEA

Ili kupata mazao mengi kutoka shambani mkulima anashauriwa kutumia mbolea aina ya samadi, mboji, maan mabichi na za viwandani
 
kwa mbolea za viwandani tumia kilo 300 au mifuko 6 za mbolea ya TSP kwa hekta moja, ns kilo 300 mifuko 6 za mbolea ya CAN au kilo 400 mifuko 8 ya SA au kilo 175 mifuko 3.5 za UREA.
 
PALIZI

Palilia viazi wiki mbili au tatu baada ya kuchomoza. inulia udongo kufanya tuta zuri ili pawepo na unyevu wa kutosha na kufunika viazi kutokana na mwanga wa jua
 
MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU

Ili kuzuia ugonjwa wa ukungu tumia Ridomil. changanya gram 100 za dawa katika lita 20 za maji na nyunyuzia mara baada kila wiki mbili au tatu kutegemea na hali ya hewa.
 
nyunyuzia dawa ya karate kiasi cha mililita 20 mpaka 40 za dawa katika lita 20 za maji ili kuzuia wadudu kama inzi weupe na wengine. Tumia mbinu bora za kilimo kama usafi wa shamba au kilimo mzunguko kama mbinu ya kuzuia magonjwa na wadudu.
 
KUVUNA NA MAVUNO

Viazi huwa tayari kuvunwa baada ya miezi 3 hadi 5 kutoka kupanda. mda wa kuvuna unategemea na muda wa kupanda na dhumuni la zao, usiache viazi shamban bila kufunika kwa nyasi au udongo kwa mda mrefu
 
KILIMO BORA CHA MINAZI

UPANDAJI
Uko wa ina mbili kuna wa vibox na wa pembetatu lakini kwa aina zote mbili umbali wa kupanda ni mita 7.6 kutoka shimo hadi shimo la mnazi, kiasi cha mashimo 175 kwa hecta huingia na kama utatumia mtindo wa pembetatu basi mashimo 13 zaidi yataingia kwa hecta.
 
Ukubwa wa shimo uwe futi tatu kwa kina, upana na urefu hi kwa maeneo yenye udongo mzuri na wakaida lakini maeneo yenye changarawe, mawe mawe na miamba ukubwa uongezeke hadi futi4 kwa mapana , urefu na kina, Shimo lijazwe majani kiasi cha kilo 15 – 20 unaweza kukisia kama theluthi moja ya shimo au futi moja baada ya kushindilia majani, weka juu yake kama, weka udongo wa juu (top soil) kiasi cha futi moja tena ongezea kiasi cha kilo 10 – 20 cha mbolea ya samadi.
 
Hakikisha haijai na kufunika shimo lote, pia kama utapata ule udongo mwekundu ambao wengi hupenda kuutumia kwenye bustani zao, pia weka humu kiasi kama utaukosa basi acha vivo hivyo, anza kumwagilia maji wiki moja kabla ya kupanda mbegu yako, kama shimo litatitia ongezea udongo wenye rutuba ya kutosha, kumbuka kuacha kisahani kwa ajili ya kukusanyia maji, ila kama ni sehemu ambazo hufurika kipindi cha mvua jaza udongo hadi kuweka tuta ili maji yasituame.
 
Back
Top Bottom