Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

watu wengi wamekuwa wanatafuta njia ya mkato, ya uhakika na isiyotumia nguvu ya kupata mafanikio kwenye maisha. Iwe ni kupata fedha, kufaulu mitihani, kutatua changamoto, kila mtu anatafuta wapi rahisi pa kupita ili aweze kupata.
 
hakuna njia rahisi, ya mkato na isiyo ya kutumia nguvu ya kupata kitu chochote chenye thamani. Lakini kama ipo njia inayokaribiana na hiyo, basi ni kujiongeza maarifa. Kama mtu atakuwa na maarifa sahihi ya kufanya kitu, basi itakuwa rahisi zaidi kwake kukifanya kuliko mtu asiyekuwa na maarifa hayo.
 
Hivyo kama unachotaka ni fedha, kuongeza kipato chako, kama una maarifa sahihi kuhusu fedha itakuwa rahisi zaidi kwako kupata na kutunza fedha zako kuliko yule ambaye hana maarifa sahihi kuhusu fedha.
 
Hivyo kama unachotaka ni fedha, kuongeza kipato chako, kama una maarifa sahihi kuhusu fedha itakuwa rahisi zaidi kwako kupata na kutunza fedha zako kuliko yule ambaye hana maarifa sahihi kuhusu fedha.
 
Kadhalika kwenye maeneo yote ya maisha, kama unataka kuwa na mahusiano mazuri, ukiwa na maarifa sahihi yanayohusu mahusiano, itakuwa rahisi kwako kuboresha mahusiano yako kuliko ukiwa huna maarifa ya aina hiyo.
 
Abraham Lincolin, aliyekuwa raisi wa Marekani, amewahi kunukuliwa akisema, akipewa masaa 6 ya kukata mti, atatumia masaa manne ya kwanza kunoa shoka lake. Na hilo halina siri, kwa sababu ukiwa na shoka kali, kazi ya kukata mti inakuwa rahisi kuliko ukiwa na shoka ambalo ni butu.
 
Hivi pia ndivyo ilivyo kwenye maisha yetu, kama una maarifa sahihi, akili yako inakuwa makini, unaweza kufanya maamuzi bora na kupiga hatua. Lakini kama huna maarifa sahihi, akili yako inakuwa butu na unashindwa kufanya maamuzi bora ya kukuwezesha.
 
Maarifa sahihi tunayapata kwa kujifunza, kupitia kusoma, kuangalia, kusikiliza na kutafakari. Lakini njia kuu kabisa, ambayo kila mmoja wetu anaweza kuitumia kwa ubora kabisa kujifunza ni kusoma. Na ninaposema kusoma simaanishi tu kusoma magazeti au makala, bali namaanisha kusoma vitabu.
 
sababu kumi kwa nini ni lazima popote unapokuwa basi uwe na kitabu. Ninaposema popote, namaanisha popote kweli, kuanzia pembeni ya kitanda chako na hata kwenye kazi yako. Na pia ninazungumzia kitabu halisi, kitabu unachoweza kushika na siyo cha kukaa kwenye simu au kompyuta.
 
Sababu ya kwanza; vitabu vinakupa maarifa.

Unahitaji maarifa sahihi ili kuweza kufanya maamuzi sahihi. Hakuna njia bora ya kupata maarifa kama vitabu. Licha ya teknolojia kubadilika na kuwa bora zaidi, bado vitabu vina thamani kubwa kuliko kitu kingine chochote. Unaposoma kitabu, unapata maarifa ambayo kama ukiyatumia, maisha yako hayawezi kubaki pale yalipo sasa.
 
Sababu ya pili; vitabu vinabadili mtazamo wako bila hata ya wewe kujua.

Watu huwa wanawaambia wenzao badili mtazamo wako kama unataka kufanikiwa. Kama vile ni kitu rahisi kusema basi kuanzia sasa nabadili mtazamo wangu! Siyo rahisi hivyo, mtazamo ambao unao, ambao umeujenga kwa miaka mingi, hautavunjika kirahisi kwa kujiambia mara moja. Badala yake unabadilika kidogo kidogo kutokana na ushahidi unaoupata kila siku kwenye maisha yako.
 
Unaposoma vitabu mara kwa mara, unalisha mawazo yako kitu fulani, sasa vitabu vinapokuwa vya aina moja, basi unaanza kujenga mtazamo unaoendana na vitabu unavyosoma. Hivyo kama unataka kutengeneza mtazamo mzuri kuhusu fedha, hebu soma vitabu kadhaa kuhusu fedha.
 
Ukitaka kujaribu usahihi wa hili, mwambie mtu anayecheza kamari au bahati nasibu kwamba njia anayotumia kutafuta fedha siyo sahihi, atakupa kila sababu kwa nini ni sahihi, au kwa nini kila kitu ni kamari. Lakini ukimfuata mtu anayesoma vitabu vya fedha na akavielewa, atakuambia kwa nini kucheza kamari na bahati nasibu ni njia ya hovyo kabisa ya kutafuta fedha.
 
kuna mtu au kampuni anaweza kunikopesha milion 100

kwa ajili ya biashara
ninacho cha kukifanya njoo pm tuzunhumze
 
Sababu ya tatu; vitabu vinakupa hoja za kutetea msimamo wako.

Ukiwa mtu wa kusikiliza vitu ambavyo watu wanavisema na wewe ukavibeba kama vilivyo na kuviamini, ni rahisi sana kubadilishwa na mtu yeyote. Kwa sababu mtu akija na hoja hata kama ni za uongo lakini anajiamini, atakufanya uone unachoamini wewe siyo sahihi.
 
Back
Top Bottom