Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sababu ya nane; kitabu kitakuepusha na majungu.

Majungu na umbeya huwa vinaanza pale watu wanapokuwa hawana kitu cha kufanya. Hivi umewahi kukuta watu walioko kwenye kazi ya dharura, inayohitajika haraka wakianza kujadili watu wengine? Huwa haitokei. Sasa kama kazi unayofanya inakupa nafasi ya kuwa na muda mwingi wa kutokuwa na kazi, basi kuwa na kitabu kunakuepusha na majungu.
 
Sababu ya tisa; kitabu kitawafanya watu waheshimu muda wako.

Watu wakiona mtu anatumia simu, huwa wanasema anachezea simu, hasa kama huonekani unaongea na simu, basi kushika kwako simu tu, watu wanajua labda upo kwenye mitandao ya kijamii au unafanya mambo yasiyo muhimu. Hata kama umeshika simu na unasoma kitabu, ni vigumu kuwashawishi watu unasoka kitabu.
 
Lakini unaposhika kitabu na ukawa unasoma, mara moja watu wanaanza kuthamini muda wako. Huwezi kusikia mtu anasema aliyeshika kitabu anachezea kitabu. Hivyo watu wanaheshimu muda wako, na siyo rahisi kuja kwako kwa jambo ambalo siyo muhimu
 
Sababu ya kumi; kitabu kitakupa njia mbadala.

Ukiwa unafanya kitu, halafu ukakwama na kila ukifikiria hupati njia, pumzika kitu hicho kwa muda na chukua kitabu usome. Hata kama kitabu hicho hakihusiani na kile unachofanya, wewe ondoa mawazo yako kwenye kile unachofanya na yaweke kwenye kitabu unachosoma. Siyo muda mrefu utapata njia ya kufanya kile ambacho umekwama.
 
[emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124]

c01a0217-934c-441f-a5c7-d9df1e0d5991.jpg
 
Back
Top Bottom