Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Chaji Simu yako huku umewasha (Flight Mode)
Sehemu ya flight mode ipo kwenye kila simu, sehemu hii itakusaidia kuzima network kwenye simu yako ya pale unapokua unataka kutumia simu yako bila kuwa na mawasiliano ya kimtandao. Sasa ukichaji simu yako uku umewasha sehemu hii inaruhusu simu yako kujaa chaji vizuri kwani chaji inayo ingia haitumiki kwa kasi kubwa na hivyo battery kujaa chaji kwa haraka zaidi na kikamilifu.
 
Hakikisha Simu yako Inaisha Chaji Ndipo Uchaji Tena
Hakikisha smu yako inaisha chaji ndipo uchaji tena, njia hii ni muhimu sana kwani inasaidia battery yako kuweza kudumu zaidi kwani kuisha kwa battery yoyote ndipo kunapo tegemeana sana na kudumu kwa chaji ya battery.
 
Yaani fikiria hivi, “maji yakikaa sana huaribika na ili kupata maji fresh ni vyema umwage kwanza yake yalio kaa kwa muda mrefu na ndipo uweke maji mengine masafi, kwa mtindo huo maji hayo mapya yatadumu zaidi kuliko kuongezea maji masafi juu ya maji ambayo yalikuwa yamesha kaa kwa muda mrefu” hivyo ndivyo battery ya simu inavyo fanya kazi, hakikisha angalau kila baada ya siku mbili una hakikisha battery ya simu yako inaisha kabisa ndipo uchaji upya.
 
Usichaji Simu yako Kwenye Joto Kali
Kwa wale ambao mnaishi Dar es salaam, najua kuwa joto ni kali ndio maana hapa Dar es salaam simu nyingi zinaharibika battery kuliko hata mikoani, japo kuwa hii inategemeana na ubora wa battery lakini ni kweli kuwa kuchaji battery mahali kwenye joto kali sana husababisha battery ya simu yako kuharibika haraka.
 
Punguza Matumizi ya Programu Zisizokuwa na Ulazima
Kama kwenye simu yako ya tecno kuna programu nyingi basi ni lazima simu yako itakuwa inaisha chaji mara kwa mara. Ili kuhakikisha kuwa battery ya simu yako ya tecno inadumu zaidi hakikisha unaondoa programu zisizo na ulazima na acha zile ambazo una matumizi nazo ya kila siku. Unaweza kuondoa programu ambazo huzitumii kila siku na pale unapo ziitaji unaweza kuzipakua tena kuliko kubaki nazo kwenye simu bila matumizi ya muhimu ya kila siku.
 
Hakikisha Bluetooth, GPS (Location) na Wi-Fi Zimezimwa
Programu nyingi mbalimbali huwa na uwezo wa kuwasha GPS au Location bila hata wewe kujua, sasa mara nyingi unapo maliza kutumia programu hizi GPS huendelea kuwaka hivyo kutumia kiasi kikubwa sana cha data, pamoja na chaji bila hata wewe kujua. Hii ni moja kati ya zile sababu kwanini unakuta kifurushi chako cha data au (Bando) kimeisha bila hata wewe kutumia.
 
Na hayo ndio mambo ambayo ni ya msingi sana kuyafanya kama unataka simu yako ya tecno iweze kudumu na chaji, baadhi ya mambo unaweza kuyafanya kwenye simu yoyote ya Android ili kuweza kuongeza ufanisi wa battery yako pamoja na kudumu kwa chaji kwa simu yako.
 
njia ya kisasa ya kujua kama simu yako ya Tecno ni original ikiwa pamoja na jinsi ya kuangalia kama battery ya simu yako ya Tecno ni original, hii ni kwa wale ambao simu zao zinafunguka mifuniko ya sehemu ya battery.
 
Kama tunavyojua tecno ni moja kati ya simu zinazo tumika sana hasa hapa Afrika na Tanzania kwa ujumla, lakini kutokana na simu hizi kuwa na wateja wengi kuna wakati wafanya biashara wasiokuwa waaminifu hutumia njia zisizo za alali kuleta na kuuza simu za Tecno ambazo sio Original
 
njia rahisi sana na ya uhakika ya kuangalia simu ya Tecno pamoja na battery yake kama ni Original, njia hii ni rahisi sana kutumia na unaweza kuifanya wakati wowote pale unapokua unataka kununua simu ya tecno au hata pale unapotaka kununua battery ya simu yako ya Tecno.
 
Kwa kuanza basi ni mahitaji ni lazima uwe na internet angalau hata MB 10, haijalishi unatumia kifaa gani iwe simu au kompyuta unaweza kufanya hatua hizi kwa urahisi kabisa, kisha kama unataka kuangalia kama simu yako ya Tecno ni Original basi fuata hatua hizi.
 
Hatua ya kwanza ingia kwenye ukurasa huu (bofya hapa) > Genuine Check kisha chukua simu yako ya Tecno kisha soma namba ya IMEI Code ( una weza kupata IMEI Code kwa kubofya *#06# kwenye simu yako ya Tecno) pamoja na namba nyingine ya VC code kisha ingiza namba hizi kwenye ukurasa wa Tecno ulio fungua awali kisha bofya Submit.
 
Baada ya hapo utaletewa maandishi ya kukwambia kama simu yako ni Original au ni feki, njia hii ni rahisi kutumia na ni ya haraka. Vilevile kama unataka kuangalia kama battery ya simu yako ya Tecno ni Original unaweza kutembelea ukurasa ule ule Genuine Check, kisha kwa chini utaona maneno Genuine Battery Check chukua battery yako ya simu ya Tecno kisha soma namba zilizo andikwa SN code kisha ziandike kwenye sehemu ya Genuine Battery Check, baada ya kumaliza bofya Submit baada ya hapo utaletewa maelezo ya kukwambia kama battery ya simu yako ya Tecno ni Original au feki.
 
Back
Top Bottom