Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mkuu wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Nacte, Dk Annastella Sigwejo katika mkutano na waandishi wa habari amebainisha kuwa walifanya uhakiki kwa vyuo 459, kati ya hivyo, 266 ndivyo vimekidhi vigezo vya kutoa elimu kwa kiwango kinachotakiwa.

Kutokana na hali hiyo vyuo vinavyoruhusiwa kudahili wanafunzi kwa ajili ya kozi mbalimbali ngazi ya astashahada na stashahada kwa muhula wa udahili wa Machi na Aprili mwaka huu vimetangazwa kwenye tovuti ya Nacte.
 
Alibainisha kuwa vyuo vilivyosajiliwa vipo 580 waliamua kujiridhisha kwa kuvifanyia uhakiki na walifanya kwa vyuo 459.

Baraza limewashauri wanafunzi kuhakikisha wanajiridhisha kwa kupata taarifa na kujiunga kwenye vyuo vilivyokidhi vigezo.
 
Mkuu wa Kitengo cha Udahili wa Nacte, Twaha Twaha amefafanua kuwa majina ya vyuo vilivyoruhusiwa kudahili yamewekwa kwenye tovuti ya Nacte. “Hivyo Nacte inashauri waombaji wa udahili kujiridhisha kwa kuangalia hiyo orodha iwapo chuo anachokitaka kinaruhusiwa kudahili,”alisema.
 
Anasisitiza kuwa ni jukumu la mzazi au mlezi kudadisi taarifa sahihi za chuo husika, hata kupitia tovuti atapata taarifa zinazomwezesha kuwa na uhakika wa uhalali wa masomo yanayotolewa hapo.

Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Omari Mbura anasisitiza chuo kujisajili kabla ya kutoa elimu ni hatua mojawapo ya kutimiza vigezo vya uhakika wa elimu inayotolewa.
 
Anasema Nacte inapaswa kuvitaja vyuo vyote vinavyobainika kutosajiliwa, hii itakuwa ni hatua nzuri ya kuwashtua wazazi na kuwafanya wawe makini.

Dk Mbura, ambaye pia ni miongoni mwa wakaguzi wa vyuo anaeleza kuwa kuna vyuo vyenye mazingira mabaya hayafai kwa elimu, ikiwamo kukosa vifaa vya kufundishia.
 
Mmiliki wa Chuo cha Ngwanza Polytechnic cha Mwanza, Jerry Nyabululu kilichozuiliwa kudahili msimu huu, anasema hatua ya udahili wa wanafunzi inasaidia kupatikana wanafunzi wenye sifa, licha ya kwamba baadhi ya wamiliki wanaiona kuwa ni changamoto
 
Naamini utaratibu huu wanaofanya Nacte ungekuwa umeanza mapema pengine hata idadi ya wafanyakazi waliofoji vyeti ambao wameng’olewa kwenye nafasi mbalimbali za kazi serikalini pengine isingekuwa kubwa, binafsi nimeuelewa kama mdau mpenda maendeleo, naunga mkono,” anasema Nyabululu.
 
Katibu mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leornard Akwilapo akizungumzia hatua hiyo iliyotangazwa na Nacte alieleza kwa kifupi kuwa ingawa bado hajaipata taarifa, lakini taasisi hiyo inatekeleza sera zinazosimamiwa na wizara hiyo.
 
Kwa mujibu wa Sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 2014 iliyozinduliwa mwaka 2015 katika ukurasa wa 24 na 25 inabainishwa kuwa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi lina jukumu la kuratibu ithibati na uthibiti wa ubora wa elimu katika vyuo vya elimu ya ufundi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…