Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IKipa wa Chelsea Thibaut Courtois amesema bado atakuwa Stamford Bridge msimu ujao hata kama hakutakuwa na maafikiano kuhusu mkataba mpya. Mkataba wa sasa wa mlindalango huyo wa miaka 25 kutoka Ubelgiji unamalizika Juni 2019. (Sporza kupitia Telegraph)
 
Chama cha Soka England FA kinapanga kuwa kikichunguza mechi zote ambazo timu taifa hilo itakuwa incheza Ijumaa usiku baada ya mashabiki wa taifa hilo kuzua fujo Amsterdam wiki iliyopita. (Times)
 
Kiungo wa kati wa Watford Abdoulaye Doucoure amesema ni ndoto yake kuchezea klabu ya Liverpool. Mfaransa huyo wa miaka 25 amehusishwa na kuhama klabu hiyo ya Vicarage Road. (Express)
 
Kiungo wa kati wa Leicester City Andy King ataruhusiwa kuondoka klabu hiyo mwisho wa msimu. Mwingereza huyo wa miaka 29 alijiunga na Swansea kwa mkopo Januari na anapangiwa kuhamia klabu hiyo ya Wales kwa mkataba wa kudumu Wales. (Leicester Mercury)
 
Pierre-Michel Lasogga ambaye yupo Leeds United kwa mkopo amesema hataki kurejea klabu yake ya Hamburg huku akiendelea kukimbiza ndoto yake ya wakati mmoja kuchezea Ligi ya Premia. Mshambuliaji huyo kutoka Ujerumani ambaye ana miaka 26 amefunga mabao 10 tangu ajiunge na Leeds mwaka jana. (Bild)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…