Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Justin Kluivert - mtoto wa Patrick Kluivert

Timu: Ajax

Mmojawapo kati ya vijana matata kabisa kwenye kikosi cha Ajax. Justin Kluivert ameonyesha dalili zote za kufuata nyayo za baba yake kwa kuwa mshambuliaji hatari licha ya umri wake kuwa na miaka 18 tu kwa sasa.
 
Akianza kuichezea Ajax mwaka msimu uliopita tu, Justin amecheza mechi 50 kwenye kikosi hicho na kufunga mabao 10. Siku za karibuni alihusishwa na Manchester United, lakini baba yake amemtaka akajiunge na Barcelona. Enzi zake Kluivert aliichezea pia Ajax na Barcelona, huku akiifanya Uholanzi kutisha kwenye soka la dunia. Alifunga mabao 199 katika maisha yake ya soka la klabu.
 
Drogba amebaki kuwa kwenye kumbukumbu za kudumu katika klabu ya Chelsea baada ya kile alichokifanya katika kikosi hicho alipoisaidia kubeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Drogba amebeba Ligi Kuu England mara nne na Kombe la FA mara nne.
 
Timothy Weah - mtoto wa George Weah

Timu: Paris Saint-Germain

Akikulia Marekani, Timothy Weah alihamia Ufaransa mwaka 2014 na kwenda kuichezea Paris Saint-Germain kabla ya kusajiliwa kwenye kikosi cha kwanza miaka mitatu baadaye.
 
Akicheza sehemu kubwa zaidi kwenye mechi za rizevu na timu za vijana, straika huyo mwenye umri wa miaka 18 alicheza mechi yake ya kwanza katika kikosi cha kwanza mwezi huu wakati alipoingia kutokea benchi kwenye mechi ya ushindi wa mabao 2-0 iliyopata PSG dhidi ya Troyes
 
Giovanni Simeone - mtoto wa Diego Simeone

Timu: Fiorentina

Panga pangua anaanzishwa kwenye kikosi cha Fiorentina msimu huu. Straika, Giovanni Simeone ameonyesha kipaji kikubwa kwamba atakwenda kuwa mshambuliaji mmoja mkubwa sana katika klabu za Ulaya.
 
Amefunga mabao saba kwenye Serie A msimu huu na tayari jina lake linahusishwa na mpango wa kwenda kujiunga na Atletico Madrid, timu inayonolewa na baba yake, Diego Simeone. Diego Simeona aliwahi kusema mchezaji ambaye atapenda sana kumnoa ni mwanaye, Giovanni.
 
Ianis Hagi - mtoto wa Gheorghe Hagi

Timu: FC Viitorul

Akiungana kwenye kundi la wachezaji watoto wa wachezaji, Ianis Hagi kwa sasa anakipiga katika kikosi cha FC Viitorul ya huko Romania, ambayo inanolewa na baba yake, Gheorghe Hagi. Alinaswa kwenye uhamisho wa Januari mwaka huu, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19, Ianis alijiunga na timu ya baba yake baada ya kushindwa kufanya mambo ya maana huko Fiorentina inayoshiriki Ligi ya Serie A.
 
Alipotua tu Viitorul, amechaguliwa kuwa nahodha. Baba yake, Hagi alicheza Real Madrid na Barcelona na alibeba mataji mengi tu Galatasaray na Steaua Bucharest. Soka la kimataifa amecheza mechi 125 na kufunga mabao 35 akifungana na Adrian Mutu.
 
Niall anacheza kwenye Ligi Kuu Scotland akikitumikia kikosi cha Partick Thistle, lakini ni baada ya kudumu kwa miaka minne katika timu ya Reading. Kwenye soka la kimataifa, Niall anaichezea Jamhuri ya Ireland, lakini bado hajaanza kukichezea kikosi cha wakubwa.
 
Back
Top Bottom