Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

JORDAN

RHODES - 2009

Mechi: Huddersfield 4-0 Exeter

Ilikuwa kwenye ligi kule Uingereza League One, ambapo takwimu kama hizi huwa nadra sana. Kwenye mechi hiyo straika Rhodes alifunga hat trick ya kasi zaidi katika historia ya soka.
 
Rhodes alitumia dakika nane tu kufunga mabao matatu. Lakini kando na kuwa mabao ya kasi, kitu spesheli zaidi ni kuwa mabao yote aliyafunga kwa kichwa.
 
SALAMON

RONDON - 2016

Mechi: West Broma 3-1 Swansea FC

Mwaka juzi straika Rondon alitumia dakika 13 pekee kuipa ushindi West Brom katika mchezo wa Ligi Kuu England. Kitu kitamu zaidi mabao yote hayo aliyapachika kwa kichwa. Ndio hat trick ya kichwa pekee katika miaka ya hivi karibuni kusajiliwa.
 
Licha ya hilo, takwimu zinazomweka kwenye kumbukumbu ni hat trick ya kichwa dhidi ya Bolton iliyoisaidia timu yake kuepuka tishio la kushushwa daraja, hali iliyokuwa ikiwakodolea macho. Mpaka leo ni yeye tu na Rondon wenye rekodi hiyo kwenye EPL.
 
TOMAS

SKUHRAVY - 1990

Mechi: Czechslovakia 4-1 Costa Rica

Ni kwenye Kombe la Dunia hatua ya 16 bora ambapo Tomas alijitambulisha duniani kwa kufunga mabao matatu ya kichwa na kulisaidia taifa lake kufuzu hatua ya robo fainali. Czechslovakia miaka mitatu baadaye iligawanyika na kuwa mataifa mawili Czech Republic na Slovakia.
 
MIROSLAV

KLOSE - 2002

Mechi: Ujerumani 8-0 Saudi Arabia

Kwenye Kombe la Dunia mwaka huu hatua ya makundi, Klose straika tegemeo wa Ujerumani alizidisha mabao yake katika dimba hilo kwa kufunga matano dhidi ya Saudi. Kati ya mabao hayo matano, matatu yalikuwa ni kupitia kichwa. Rekodi hii ya kufunga hat trick ya kichwa kwenye Kombe la Dunia anaishikilia yeye na Skuhravy pekee mpaka leo.
 
EDINSON

CAVANI - 2011

Mechi: Napoli 3-0 Juventus

Ulikuwa ni msimu wa kwanza wa Cavani straika wa Uruguay (sasa yuko PSG), katika Ligi Kuu ya Italia, Serie A dhidi ya Juventus. Cavani aliipa ushindi Napoli kwa mabao matatu kupitia kichwa ijapo bao la mwisho lilizua utata ikiwa aliupachika kwa kichwa au mguu wake kwa sababu aliinamisha kichwa na wakati huo akiwa amenua mguu vilevile.
 
KLAAS JAN HUNTELAAR - 2007

Mechi: Ajax 8-1 De Graafschap

Akiwa kwenye msimu wa mwisho Uholanzi msimu wa 2007/2008 kabla ya kuhamia Real Madrid kisha Schalke 04 Ujerumani, Huntelaar aliifedhehesha De Graafscha mabao manne. Katika mechi hiyo Huntelaar alipachika matatu kwa kichwa.

Bao lake la mwisho katika mchezo huo lilitokana na penalti.
 
Miongoni mwao kama Kasper Schmeichel au Daley Blind, wote hao wamefanya vizuri kufuata nyayo za baba zao na kupata mafanikio makubwa kwenye soka wakicheza klabu zinazojielewa kwenye Ligi Kuu England, mmoja akiwa Leicester City na mwingine Manchester United.
 
Miongoni mwao kama Kasper Schmeichel au Daley Blind, wote hao wamefanya vizuri kufuata nyayo za baba zao na kupata mafanikio makubwa kwenye soka wakicheza klabu zinazojielewa kwenye Ligi Kuu England, mmoja akiwa Leicester City na mwingine Manchester United.
 
Back
Top Bottom