Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa mfano unamuuliza mtu jana ulikuwa saa saba mchana ulikuwa wapi? Yeye anaanza kukuambia ujue jana nilibanwa kweli, nilikuwa nimeenda … nikakuta… halafu… Angalia kwa makini, swali ni ulikuwa wapi, lakini majibu hayajibu wapi. Hapo mtu hana uhakika, hajui au anadanganya.
 
Ukitaka kupima hilo vizuri, angalia mwanasiasa anapoulizwa swali, iwe ni wananchi au hata kwenye mahojiano. Mfano anaulizwa, umeahidi kujenga barabara eneo fulani, ujenzi huo unaanza lini? Majibu utasikia yanaanza na pale upembuzi yakinifu utakapofanyika na mchakato wa kuwashirikisha wadau ukikamilika basi mradi utaanza mara moja.
 
Ukiangalia hapo, swali halijajibiwa, lakini aliyepokea maelezo hayo ataridhika, halafu hatakuwa na kitu cha kumshika, kwa sababu hajaahidi tarehe kamili ya kuanza, na ameweka mambo mengi ambayo hujui yatakamilika lini. Hujui mchakato na upembuzi utakamilika lini na hivyo huwezi kumdai kwenye hilo.
 
Ukiangalia hapo, swali halijajibiwa, lakini aliyepokea maelezo hayo ataridhika, halafu hatakuwa na kitu cha kumshika, kwa sababu hajaahidi tarehe kamili ya kuanza, na ameweka mambo mengi ambayo hujui yatakamilika lini. Hujui mchakato na upembuzi utakamilika lini na hivyo huwezi kumdai kwenye hilo.
 
Siyo lazima umwambie mtu anadanganya, lakini mbinu hii itakusaidia kuwa na imani na majibu ya watu au la. Na kwa upande wa pili, unapoulizwa kitu jibu, na kama kuna maelezo ya ziada yatoe baada ya kutoa jibu la uhakika. Usizunguke na maneno mengi, wanaoelewa watajua unadanganya na hawatakupa uzito kwenye kile unachosema au kuahidi.
 
Kunakuwa na kitu ambacho kinachochea tabia kufanyika, halafu kichocheo hicho kinamsukuma mtu kufanya TENDO fulani na mwishowe anapata zawadi.

Sasa ni hiyo zawadi ndiyo inamfanya mtu kuendelea kufanya kitendo kile zaidi na zaidi.
 
Kwa mfano, kwa mtumiaji wa madawa ya kulevya, pombe au sigara, kichocheo kinaweza kuwa kujisikia vibaya, kuwa na msongo wa mawazo, kushindwa kitu fulani au hata kuwa na mgogoro na wengine. Hali hizo zinamchochea mtu kuondokana nazo kwa haraka.
 
Anaamua kutumia ulevi wake, labda madawa ya kulevya, pombe au sigara. Kwa kutumia ulevi huo, kwa muda anajisikia raha, anasahau kabisa yale yaliyokuwa yanamsumbua, na kwa muda anakuwa huru, bila ya usumbufu wowote kimawazo.
 
Sasa hili lingekuwa bora, kama hali hiyo ingedumu kwa muda wote wa matatizo ya mtu huyo. Lakini tatizo ni kwamba, hali hiyo inadumu kwa muda mfupi mno, haizidi masaa. Hivyo hali hiyo ikipita, mtu anarudi kwenye hali yake ya awali, tatizo liko pale pale, na hilo linamchochea kutumia zaidi. Anatumia tena, anajisikia vizuri kwa muda, lakini baada ya muda inaisha, matatizo yako pale pale, anasukumwa kutumia tena. Hivi ndivyo mtu anaishia kuvuta sigara 20 kwa siku, au kunywa pombe kila siku, au kutumia madawa ya kulevya kila mara.
 
1522185253901.gif
 
Kwa mwenendo huo, inafika mahali sasa mwili hauwezi tena kufanya kawaida bila ya kile kilevi ambacho mtu amezoea, na hivyo akijaribu kuacha, anajisikia vibaya zaidi na hivyo kujikuta akilazimika kuendelea, licha ya kwamba kitu kina madhara kwake. Na hapo ndipo tunasema mtu huyo amekuwa mteja.
 
Aina hizo ni kama ifuatavyo;

Uraibu kwenye teknolojia, hasa mitandao ya kijamii.

Uraibu kwa mtu mwinyewe, yaani unakuwa mteja wa mawazo yako mwenyewe kiasi kwamba inakuzuia kuziona fursa zaidi.

Uraibu kwenye kelele, hasa kwenye matumizi ya simu, hizi simu janja aka smartphone.
 
Uraibu kwenye mapenzi.

Mwandishi pia ameelezea kemikali muhimu sana ambayo inahusika kwenye kutengeneza uraibu ambayo ni kemikali ya dopamine.

Mwisho kabisa mwandishi ameeleza njia za kuepuka kuingia kwenye uraibu na hata kujiondoa kwenye uraibu.
 
Back
Top Bottom