Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuna wakati hasira inaweza kuwa imetokana na wasiwasi, na hapa ndipo unatakiwa uchunguze hasira uliyonayo imetokana na nini? Je imetokana na asili yangu ya kuwa na hasira kila wakati au? Je imetokana na wasiwasi? Je kinachosababisha niwe na hasira ni cha kweli au ni wasiwasi wangu tu?
 
Kuna wakati hasira inaweza kuwa imetokana na wasiwasi, na hapa ndipo unatakiwa uchunguze hasira uliyonayo imetokana na nini? Je imetokana na asili yangu ya kuwa na hasira kila wakati au? Je imetokana na wasiwasi? Je kinachosababisha niwe na hasira ni cha kweli au ni wasiwasi wangu tu?
 
Je kuna mazoea ambayo nimejiwekea ambayo yanapelekea hasira hii? Ni vyema kufahamu hayo kwani unaweza kukuta hasira uliyonayo imetokana na hisia tu na sio uhalisia. Unaweza ukachunguza na kufahamu kuwa kumbe ilikuwa haina haja ya kuwa na hasira.
 
Tambua kuwa hasira haimuumizi tu mtu anayeishikilia bali mpaka na maisha yake.

Kuna watu wao wameshajichukulia kuwa hasira ni hasira tu. Wao hasira ikiwatokea wanajisahau na kuanza kutenda mabaya kama vile kulipiza kisasi kwa waliomkosea,
 
Pia kuishikilia hasira unajinyima raha na uhuru, unaanza kutumia muda wako kuwaza badala ya kuutumia muda wako kufurahia uhai wako na kushukuru kwa kila jambo.
 
Hasira ikikuanza, ipe muda kwanza kabla ya kufanya maamuzi.

Pale hasira inapokutokea ni vyema kutokuwa mwepesi kuisikiliza hasira yako. Hasira muda wote huja na jibu au tendo linalokushawishi ulitende. Mara nyingi jinsi hasira inavyochemka na maamuzi yake nayo yanakuwa mabaya na hasira inapopoa uamuzi wake angalau unakuwa sio mbaya sana.
 
Kama hasira ikikuanza na ukaona unaweza kufanya maamuzi mabaya ni vyema kuipa muda, usikubali kufanya maamuzi ya haraka. Itakusaidia kutafakari kwa kina na labda kama kuna kitu ulikuwa haukifahamu kinaweza kujidhihirisha na kuweza kufanya hitimisho sahihi.
 
Jifunze kukubaliana na hali.

Wengi ambao ni wagumu sana kukubaliana na hali ni wepesi sana kuwa na hasira. Kuna wakati hasira hutokana na mategemea, unategemea tokeo fulani au kitu fulani halafu mambo yanakuwa tofauti.
 
Hasira inakushawishi usikubali, na jinsi unavyozidi kutokukubaliana na hali ndipo unazidi kuwa mtumwa wa hasira yako. Kuna hali ambazo hasira ikikujia, ukiamua kukubaliana na hali na hasira nayo inaondoka. Wengi wanashikilia vitu, umaarufu, mali, sifa, n.k na kushindwa kuviachia.
 
Jifunze kuacha mambo yaende kama yalivyo Jifunze kukubaliana na maisha katika hali zozote. Kubali kuwa hujaja na chochote hapa duniani na hutaondoka na chochote, jiweke huru kwa lolote. Utaona maajabu yake pale utakapoamua kuishi kama mtoto mdogo asiye na hasira kwani ni mwepesi kukubaliana na hali, atalia tu akiona hali sio nzuri kwake lakini baada ya muda anasahau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…