Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwenye kikosi cha Russia msimu huu, kuna staa anaitwa Alexsandr Golovin, ambaye kimsingi anatazamwa atakwenda kufanya mambo ya maana ambayo hakika yatamfanya awe na dili kibao kwenye meza yake zinazohusu usajili. Timu anayochezea Golovin kwa sasa ni CSKA Moscow. Umri wake ni miaka 21 tu na kiungo huyo ana kipaji kikubwa kinachomfanya kuwindwa na timu za maana kama Barcelona na Arsenal.
 
6.Timo Werner

(RB Leipzig)

Mabao yanalipa kodi unaambiwa. Ndiyo wanavyosema. Na Timo Werner amekuwa mwenye furaha kubwa kabisa kwa sababu kama angekuwa mpangaji, basi asingekuwa na shida na mwenye nyumba wake kutokana na anavyofunga mabao, ambayo angeweza kuyatumia kulipia kodi ya pango.
 
Vionjo vya Ferouz kwa mbali...Halafu dogo sembe imempoteza. Mungu Amsaidie apone...
 
7.Eden Hazard (Chelsea)

Ni mmoja wa mastaa wakubwa kabisa kwenye Ligi Kuu England kwa sasa na si jambo la kificho, Hazard ataendelea kutajwa kwenye kila dirisha la usajili litakapofika hadi hapo atakapohama Chelsea na kwenda kwenye timu nyingine.
 
Kwenye fainali za Kombe la Dunia, Hazard atakwenda kucheza sambamba na Kevin De Bruyne na bila ya shaka matarajio ni makubwa kwamba atakwenda kung’ara katika fainali hizo. Kwa sasa habari kubwa kuhusu staa huyo ni kwamba anasakwa na Real Madrid na kuna uwezekano mkubwa akaachana na Chelsea mwishoni mwa msimu huu na kwenda kuanzisha mapinduzi huko Santiago Bernabeu, ambako mabosi wamepania kufanya usajili mkubwa kabisa mwishoni mwa msimu huu.
 
Kwenye fainali za Kombe la Dunia, Hazard atakwenda kucheza sambamba na Kevin De Bruyne na bila ya shaka matarajio ni makubwa kwamba atakwenda kung’ara katika fainali hizo. Kwa sasa habari kubwa kuhusu staa huyo ni kwamba anasakwa na Real Madrid na kuna uwezekano mkubwa akaachana na Chelsea mwishoni mwa msimu huu na kwenda kuanzisha mapinduzi huko Santiago Bernabeu, ambako mabosi wamepania kufanya usajili mkubwa kabisa mwishoni mwa msimu huu.
 
8.Jack Wilshere

(Arsenal)

Bado anahesabika kuwa ni mmoja kakti ya viungo bora kabisa waliowahi kutokea kwenye soka la England.

Jack Wilshere bado hajacheza kwa kiwango bora kabisa cha soka lake kutokana na muda mwingi anapocheza na kukaribia ubora wake amekuwa akipatwa na majeraha
 
Mashabiki wa Arsenal wanakumbuka nyakati zile ambazo Wilshere alikuwa kwenye ubora wake na kuwafunika viungo wa Barcelona uwanjani mwaka 2011 na imani ni kubwa kwamba kuna siku kutaonekana Wilshere yule wa wakati ule.
 
Fainali zijazo za Kombe la Dunia zitakuwa nafasi yake ya kwenda kuonyesha kiwango bora ili kupata timu ya kwenda kujiunga nayo baada ya Arsenal kuonekana kutokuwa na mpango wa kumwongezea dili jipya kutokana na hilo la sasa kutarajia kufika tamati mwishoni mwa msimu
 
9.Sergej Milinkovic-Savic (Lazio)

Jina lake halina nguvu sana, lakini usiambiwe, Milinkovic-Savic ni bonge la mchezaji na timu itakayofanikiwa kunasa huduma yake itakuwa imepiga bonge la usajili. Inaelezwa Manchester United ndio inayopewa nafasi ya kunasa saini yake kwenye dirisha lijalo la usajili na kinachoelezwa ni kwamba staa huyo wa Serbia anayekipiga kwenye kikosi cha Lazio, anaelezwa kwamba ni mmoja kati ya wakali wenye vipaji vikubwa sana waliowahi kutokea kwenye Serie A.
 
Amepachikwa jina la Sajenti kutokana na namna anavyowapa shida wapinzani kwenye sehemu ya kiungo na staili yake ya uchezaji imemfanya alinganishwe na staa wa zamani wa Inter Milan, Dejan Stankovic. Milinkovic-Savic ni moja ya sura ambazo hutarajii kuziona zikibaki kwenye timu zao wanazochezea kwa sasa itakapofika msimu ujao.
 
10.Andre Silva (AC Milan)

Kama ilivyo kwa Timo Werner, Andre Silva ni mtambo wa mabao. Alifunga mabao tisa katika mechi za Ureno za kufuzu kwa Kombe la Dunia na kitu cha kuvutia ni kwamba bado mshambuliaji kijana sana kutokana na kuwa na umri wa miaka 22 tu. Kiwango cha kwenye klabu yake kinatia mashaka kidogo. Licha ya kwamba amefunga mabao sita kwenye mechi nane alizoanzishwa kwenye Europa League akiwa na AC Milan, kwenye Serie A amefunga mara mbili tu.
 
Amekuwa akitumika zaidi kama mshambuliaji wa kutokea benchi kuliko kuanza, lakini kwa mwenendo wa AC Milan, Silva anaweza kuchukua uamuzi tofauti na kuamua kutimkia kwenye Ligi Kuu England mahali ambako kuna timu kibao zimeripotiwa kuhitaji huduma yake.
 
11.Emil Forsberg

(RB Leipzig)

Si jina kubwa sana, lakini kiwango chake kinamfanya awe kwenye mipango ya timu mbalimbali zinazochuana kuwania huduma yake. Ni staa wa RB Leipzig na kiwango chake bora cha msimu huu kinamweka kwenye nafasi ya kuwa mmoja wa wachezaji ambao kuwaona wakiendelea kubaki kwenye timu hiyo hadi msimu ujao basi itakuwa bahati kubwa sana.
 
Forsberg ni msumbufu sana ndani ya uwanja na kiungo huyo mshambuliaji umri wake ni miaka 26 na hakika yupo kwenye kiwango bora cha soka lake. Kwa kipindi hiki ambacho Zlatan Ibrahimovic hana maajabu kwenye kikosi cha Sweden, Forsberg amebaki kuwa tumaini la timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia. Arsenal wanamhitaji.
 
12.Robert Lewandowski

(Bayern Munich)

Kuna ambaye hafahamu kwamba Lewandowski ni mmoja kati ya washambuliaji wa kati wenye uwezo mkubwa sana wa kutikisa nyavu duniani. Kwa sasa yupo kwenye kikosi cha Bayern Munich, licha ya kwamba hana uhakika wa maisha katika timu hiyo wababe wa Bundesliga. Akiwa na umri wa miaka 29, Lewandowski bado anaweza kubamba dili la maana katika kumalizia maisha yake ya so
 
Klabu kadhaa za Ligi Kuu England zinamtaka sambamba na Real Madrid na jambo hilo linaweka uwezekano mkubwa wa fowadi huyo wa kimataifa wa Poland kuachana na Bayern Munich mwishoni mwa msimu huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…