Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Boga ni zao ambalo mmea wake unakuwa kwa kutambaa na ni la mviringo, ngozi yake ni nyororo na rangi yake ni ya njano inayoelekea kwenye rangi ya chungwa au rangi ya kijani. Katikati ya boga kuna mbegu na massa, Boga lipo katika jamii ya Cucurbita pepo.
Ahsante kwa elimu nzuri kuhusu kilimo cha maboga.
Ubarikiwe sana.
ASILI YAKE
Asili ya boga ni Amerika kaskazini, maboga yamekuwa yakipandwa kwaajili ya biashara na kwaajili ya chakula. Kwa sasa maboga yamekuwa yakilimwa maeneo mbalimbali duniani, Antarctika pekee ndiko maboga hayawezi kustawi. Mataifa yanayozalisha maboga kwa wingi ni Marekani (USA), Canada, Mexico, India, and China.

HALI YA HEWA & UDONGO
Maboga yanahitaji joto la wastani kutoka kwenye jua, pia eneo ambalo halituamishi maji udongo wake uwe na pH kati ya 6.0 – 6.8. Pia udongo uwe na joto inchi tatu (sm 7.6) kushuka chini angalau nyuzi 60 °F (15.5 °C), maboga yatadhoofika kama maji yatakosekana.

UTAYALISHAJI WA SHAMBA
Shamba litayalishwe kwa umakini bila kuwa na sehemu ya kutuamisha maji maana mmea wa maboga na maboga yenyewe hutambaa chini, tumia jembe la ng’ombe, trekta, jembe la mkono au pawatila, changanyia mbolea za asili (samadi au mboji) na udongo ili kurutubisha shamba.

UPANDAJI
Maboga hupandwa kwa kufukia mbegu sentimita 1 au 2 chini ya udongo , panda mbegu 2 kila shimo. Pia panda umbali wa sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 – 2 kutoka mstari hadi mstari.

UTAYALISHAJI WA MBEGU
Mbegu za maboga zinatoka ndani ya maboga, kuna mbegu zilizoboreshwa (za kisasa) na za asili, andaa mbegu mapema wiki moja au mbili kabla ya kupanda.

MATANDAZO (MULCHES )
Kwasababu ni zao linalotambaa basi lazima tuangalie namna ya kutandaza, weka nyasi na mabaki ya mimea mingne kufunika ardhi.

Baada ya miche kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches) ambayo yaweza kuwa nyasi kavu kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko wa udongo.
 
220px-Esso_textlogo.png
 
Back
Top Bottom