Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Kwa kutazama ratiba ya Tottenham Hotspur ilivyo kwa mechi zao tatu zijazo, unaweza kuona kabisa presha inayowakabili mashabiki wao. Kwanza watashuka uwanjani Stamford Bridge leo Jumapili kucheza na Chelsea na baada ya hapo itacheza na Stoke City huko Britannia na kisha watarudi Wembley kucheza na Manchester City. Spurs itapaswa kucheza kwa akili sana na kuvuna pointi muhimu ambazo zitawafanya kuendelea kubaki kwenye Top Four. Kama mambo yatakuwa kama inavyotabiriwa, Spurs inaweza kumaliza msimu na pointi zake 77, ambazo zitawafanya kuwa juu ya Liverpool katika msimamo wa ligi hiyo na hivyo watakuwa na uhakika mkubwa wa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.