Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

29418105_434346267016940_6780733189687083008_n.jpg
 
Habari za asubuhi watu wa Mungu, naamini wote mmeamka salama na uzima pia upo ndani basi yatupasa kushukuru kwa kila jambo jema mbele yetu pia muwe na siku hii iwe njema kwenu.
 
STRAIKA Romelu Lukaku amekuwa mchezaji wa 28 kwenye Ligi Kuu England kufikisha mabao 100.

Staa huyo wa Manchester United aliweka rekodi hiyo baada ya kufunga bao katika dakika ya tano tu katika mechi ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Swansea City na kufunga bao lake la 15 msimu huu, lakini la 100 katika historia yake ndani ya Ligi Kuu England.
 
Baadhi tu ya mastaa wengine waliopo kwenye orodha hiyo ya wakali waliotupia mabao 100 wavuni ni Thierry Henry na Alan Shearer.

Bao lake Lukaku alipigiwa pasi na Alexis Sanchez, ambaye ndiye aliyefunga bao la pili kumpa raha Kocha Jose Mourinho.

Kuhusu Lukaku, alifunga mabao 100 baada ya kucheza mechi 216 katika klabu zote alizopita ambazo zilimpa nafasi ya kucheza Ligi Kuu England, West Brom, Everton na Man United.
 
Wakati alipokuwa Chelsea, Lukaku hakufunga bao kwenye mechi za Ligi Kuu England. Lakini, alipokwenda kwa mkopo, West Brom alifunga mara 17 katika mechi 35. Alirudi Chelsea na kutolewa tena kwa mkopo kwenda Everton alikofunga mabao 15 kabla ya timu hiyo kumbeba jumla na alikwenda kufunga mabao 53 katika mechi zaidi ya 110 alizoitumikia timu hiyo yenye maskani yake Goodison Park.
 
Mwanasoka nyota wa kimataifa wa zamani Nwankwo Kanu ametangaza kwamba atawania urais katika uchaguzi mkuu mwaka 2019.

Kanu, aliyewahi kuzichezea Ajax, Inter Milan na Arsenal katika ujana wake, amesema ana ndoto ya kufanya mageuzi katika taifa hili kubwa na lenye watu wengi barani Afrika.
 
Mshindi huyo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 1995 hajaficha shauku yake ya kujiingiza katika siasa tangu alipostaafu kucheza soka akiwa klabu ya Portsmouth mwaka 2012. Kanu anaweza kufuata nyayo za gwiji wa soka George Weah ambaye sasa ni rais wa Liberia.

Wakati akitangaza nia yake ya kugombea urais, Weah – mshindi wa Tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika mwaka 1996 na 1999 aliwaambia wafuasi wake kadhaa.
 
Shauku ya urais wa Kanu

“Kuwepo kwangu hapa leo kunahusu hali ya baadaye ya nchi yetu na faraja ya watu wetu,” alisema mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 41.

“Miaka 18 iliyopita ya uongozi imeshuhudiwa kuanguka kwa sekta zote kubwa katika maisha ya Nigeria, pamoja na usalama katika ardhi hii. Pia, nitafanya kila liwezekanalo kupambana na ufisadi ambao umeenea kila mahali. Dunia inaitazama Nigeria kama makazi ya ufisadi.
 
Ikiwa nitapewa mamlaka na ninyi, naahidi kufanya mambo tofauti na kurejesha heshima na maadili katika huduma za taifa kwa kuwa na watumishi bora na kuvutia walio bora.

"Ushindi wa George Weah nchini Liberia ni kielelezo kwamba ndoto hii inawezekana kwa ninyi wote kuwa upande wangu."

Kanu atakuwa anatarajiwa kuwa rais wa taifa hili ikiwa atafanikiwa kumshinda rais wa sasa Muhammadu Buhari.
 
Aliyekuwa Makamu wa Rais Mokgweetsi Masisi Jumapili aliapishwa kuwa rais mpya katika sherehe zilizofanyika jijini akichukua nafasi ya Ian Khama, ambaye ameamua kustaafu.

Masisi, mwenye umri wa miaka 55, anakuwa rais wa tano baada ya Seretse Khama, Ketumile Masire, Festus Mogae na Ian Khama.
 
Mvua kubwa ilinyesha asubuhi hiyo wakati wananchi wakisubiri kushuhudia kuapishwa kwa kiongozi mpya wa nchi. Ilionekana kwamba mvua hiyo ingeweza kuwakatisha tamaa watu lakini kinyume chake wabunge, maofisa usalama, watumishi wa mahakama na wananchi walijazana katika tukio hilo la kihistoria.
 
Kwa mujibu wa katiba ya Botswana, rais anatumikia vipindi viwili vya miaka mitano mitano na hupaswa kumkabidhi madaraka naibu wake mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu.

Masisi aliapishwa kwenye ukumbi wa Bunge na amekabidhiwa uongozi wa nchi ikiwa imebaki miezi 18 kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu Oktoba 2019.
 
Kwa mujibu wa katiba ya Botswana, rais anatumikia vipindi viwili vya miaka mitano mitano na hupaswa kumkabidhi madaraka naibu wake mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu.

Masisi aliapishwa kwenye ukumbi wa Bunge na amekabidhiwa uongozi wa nchi ikiwa imebaki miezi 18 kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu Oktoba 2019.
 
Ian Khama ambaye katika miezi ya hivi karibuni amekuwa akitoa wito kumtaka Rais Joseph Kabila ajiuzulu urais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, alitangaza tangu mwaka jana kuwa atang’atuka madarakani Aprili na kumwachia madaraka makamu wake.

Botswana haina uchaguzi wa rais wa moja kwa moja. Kiongozi wa nchi anachaguliwa na chama chenye wabunge wengi. Kwa sasa, chama tawala cha Botswana Democratic Party (BDP) ndicho chenye wabunge wengi.
 
Ian Khama ambaye katika miezi ya hivi karibuni amekuwa akitoa wito kumtaka Rais Joseph Kabila ajiuzulu urais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, alitangaza tangu mwaka jana kuwa atang’atuka madarakani Aprili na kumwachia madaraka makamu wake.

Botswana haina uchaguzi wa rais wa moja kwa moja. Kiongozi wa nchi anachaguliwa na chama chenye wabunge wengi. Kwa sasa, chama tawala cha Botswana Democratic Party (BDP) ndicho chenye wabunge wengi.
 
Baada ya kuapishwa, Rais Masisi, alisema kuwa kupunguza ukosefu wa ajira kati ya vijana, ndio jambo muhimu kabisa kwake, na pia aliahidi kuyapa kipaumbele, mapambano dhidi ya Ukimwi, ulevi na madawa ya kulevya pamoja na rushwa.
 
Kama ni mchezaji au mfanya mazoezi umewahi kujua kama unywaji pombe ni salama kwako kwa upande wa kiwango chako cha uchezaji na utimamu wa mwili wako?

Kama ulikuwa hujui, kiujumla unywaji pombe unaathiri kiwango cha mchezaji na utimamu wa mwili wake kwa njia mbili zifuatazo.

Njia ya kwanza ni kwasababu pombe huchochea figo kuruhusu maji kupotea kwa wingi kwa njia ya mkojo, hivyo unywaji wa pombe uliopitiliza unasababisha upungufu wa maji mwilini.
 
Kwa mfano mwanamichezo au mchezaji akanywa pombe kwa wingi na kisha akaingia katika zoezi au mechi, mchezaji huyu huwa katika hali mbaya zaidi kutokana na ukweli kuwa atapoteza maji mengi kwa njia ya jasho kwakuwa kadiri anavyocheza ndivyo joto la mwili hupanda na hivyo jasho hutoka kwa wingi.

Muunganiko wa kutokwa jasho na athari ya pombe ya kupoteza maji kwa njia ya mkojo huweza kuleta upungufu wa maji mkali kwa mchezaji.
 
Wakati wote mwanamichezo hutakiwa kuwa na kiasi cha maji ya kutosha mwilini ili kuwezesha mtawanyiko mzuri wa damu. Ikumbukwe kuwa damu ndiyo imebeba oksijeni na virutubisho muhimu kwa ajili ya misuli kukunjuka na kujikunja.

Hivyo basi upungufu wa maji mwilini huathiri utendaji wa misuli hivyo moja kwa moja huaathiri kiwango cha uchezaji na utimamu wa mwili kiujumla.
 
Back
Top Bottom