Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hali ya upungufu wa maji mwilini huambatana na hali ya kubanwa misuli na kupata vijeraha vya misuli kirahisi. Vile vile kama kuna majeraha huchelewa kupona.

Njia ya pili ni kuwa pombe huingilia mfumo wa utengenezaji nishati ya mwili (glucose), ikumbukwe kuwa glucose ndiyo kama petroli ya mwili inayotumiwa na misuli ya mwili kufanya kazi yake.
 
Pale unapokunywa pombe na inapoingia tumboni na kuvunjwa vunjwa au kusagwa huwa ini linashindwa kutengeneza kiasi cha kutosha cha nishati (glucose).

Hali hii ndiyo inayosababisha kuwa sukari ya mwili au nishati (glucose) katika damu kuwa chini. Mazoezi yoyote huitaji kiasi cha kutosha cha sukari/nishati ili kukupa nguvu.

Hivyo kwa mnywaji wa pombe ini lake hushindwa kutengeneza sukari/nishati hivyo mwili kukosa nguvu na hii huathiri kiwango cha mchezaji kwani atashindwa kucheza kwa nguvu.
 
Njia hizi mbili ndizo zina matokeo kama humsababishia mwanamichezo kukosa nguvu, misuli kuumwa na kuwa dhaifu, kuwa mchovu, kushindwa kuwa makini uwanjani, kukosa utulivu, kichwa kuuma, kubadilika tabia ikiwamo ukali au ukorofu na kuongezeka uzito kiholela.

Pia pombe inasababisha protini tunayoipata kwa kula vyakula kutonyonywa katika mfumo wa chakula. Kukosekana kwa kirutubisho hiki kwa mwanamichezo misuli yake haita jengeka na kuimarika.
 
Nihitimishe kwa kushauri wanamichezo kutokunywa pombe huku wanashiriki michezo, wakishindwa kuacha basi wanywe kwa kiasi. Lengo ni kulinda viwango vyao visiporomoke.
 
Back
Top Bottom