Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tabia au sifa zipi zinakusukuma jinsi ya kuishi maisha Yako?

Kama mtu atakuuliza swali hili utalijibu vipi? Hili swali sio kuhusu mwaka mpya tu, ni kitu ambacho kinahusiana na undani wa maisha yako, thamani yako, point of view, mtazamo wako wa ndani kabisa unaokusukuma wewe.
 
Mfano. Viongozi wengi wana kiwango kikubwa kuridhika na maisha pamoja na ustawi wao ni mzuri. Wana malengo makubwa ambayo wamepanga japo ni wazee, lakini vijana wengi hawako hivyo. Viongozi wanaishi kama vijana wadogo wa miaka 25, ndani ya akili zao , japo wana miaka 80.
 
Turudi kwenye swali letu. Sifa zipi zinakuvutia wewe na zinakupa msukumo mkubwa katika maisha yako? Hapa kuna baadhi ya vitu vinavyowezekana, vyenye ujasiri, vyenye wema , ukamilifu, usawa. kwa sababu tunaishi katika nyakati ambazo tunashambuliwa na taarifa nyingi, na nyingine zinatufanya kuwa na usikivu, zinatuokoa , zipo vizuri, zinalenga jinsi gani ya kukabiliana na changamoto ambazo zinatulemea, hasa ukiwa kama kijana au kiongozi.
 
1.Heshimu maisha yako, undani wako.



Utaweza kuheshimu maisha yako kwa kuwa mtu wa kutumia muda vizuri. Hasa katika kutafakari, maombi, kupata utulivu wa kipekee hata kwa dakika chache kila siku. itakusaidia kukabiliana na changamoto nyingi .Lisha akili yako taarifa sahihi.
 
2.Fanya zoezi la Kusimamisha hisia mbaya.

Acha kutazama taarifa mbaya, achana na mitandao kama haikuletei faida maishani mwako, achana na vikao mbalimbali vinavyokufanya ukose muda wa kufikiri ili kupata wazo jipya. Acha na tazama undani wako, moyo wako unakuambia nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…